Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu yaipongeza ucsaf kwa utendaji kazi

 

Mtendaji
Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba akitoa mada kwenye semina ya wabunge wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyoandaliwa na Mfuko huo
wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo
iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile
akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya
miundombinu katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu
mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso,akitoa
neno la pongezi mara baada ya kumaliza kupewa mafunzo na elimu katika
semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye
lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo
iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Baadhi
ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakitafilia
semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye
lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo
iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.



Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye ni Mbunge wa
Ilala,Mhe. Musa Azan ‘Zungu’ akichangia katika semina iliyoandaliwa na
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa
wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini
Dodoma.



Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora, Humphrey Polepole
akichangia katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu
mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.




Na Alex Sonna, Dodoma


Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema itahakikisha inashirikiana na
serikali ili Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uwe na bajeti nzuri
itakayosaidia kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbalimbali nchini
hususan yaliyopo pembezoni na mipakani.


Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Selemani Kakoso ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza
viongozi wa Wizara, Menejimenti ya Wizara na watendaji wa UCSAF katika
semina kwa wajumbe wa kamati hiyo na baadhi ya wenyeviti wa kamati za
bunge kuhusu huduma ya mawasiliano.


Akizungumza
katika kikao hicho, Kakoso ameupongeza mfuko huo kwa utendaji mzuri wa
baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine
Ndugulile kuwasilisha taarifa ya majukumu ya Mfuko huo.


Amesema wabunge wataendelea kuishauri serikali kuimarisha utendaji kazi wa mfuko huo ili kufikisha mawasiliano kwa wananchi.


Kwa
upande wake, Dk.Ndugulile alisema kikao hicho ni kuwajengea uelewa
wajumbe wa kamati hiyo ili wafahamu majukumu ya UCSAF na kushirikiana na
Wizara kuhakikisha kuwa UCSAF inatekeleza majukumu yake na kufikia
malengo iliyojiwekea.


“Wizara
hii inasimamia njia moja kuu za uchumi kama ilivyo Wizara ya Ujenzi
inavyobeba barabara na Nishati inabeba umeme, na hii ni moja ya njia kuu
za uchumi katika dunia ambayo tunakwenda nayo ili tuhakikishe kuwa
tunajenga uchumi wa kidijitali kwa kuwa sasa hivi dunia imehamia
kiganjani na Wizara hii itaratibu masuala yote ya TEHAMA ndani ya
Serikali ili mwananchi apate huduma kwa wakati na TEHAMA ichangie
kikamilifu pato la taifa,”amesema.


Naye,
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew, amefafanua kuwa
Wizara kwa kushirikiana na UCSAF na kampuni za simu za mkononi
wataendelea kuboresha huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali
nchini kwa kuongeza uwezo wa minara ya mawasiliano.


Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Humphrey Polepole
ameipongeza UCSAF kwa kujenga vituo vya TEHAMA kwenye kisiwa cha Unguja
na Pemba ambapo vituo hivyo vinawawezesha wananchi kupata huduma ya
intaneti karibu na maeneo yao na ameshauri ujenzi wa vituo hivyo
uendelee kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.


Awali,
Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mshiba amesema kuwa UCSAF itapita
kwenye maeneo yote ya mipakani mwa Tanzania na kufanya tathmini ili
kupata idadi ya minara inayohitajika kwenye maeneo hayo ili kuhakikisha
kuwa maeneo ya mipakani yana mawasiliano ya uhakika.