Kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu yawasili shinyanga kutembelea na kukagua miradi miwili ya maendeleo


Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu leo Machi
14,2024 imefanya ziara Mkoani Shinyanga ambapo imetembelea na kukagua Mkongo wa
Taifa katika shirika la  mawasiliano Tanzania
(TTCL) mjini Shinyanga pamoja na mradi katika ukarabati na uboreshaji wa kiwanja
cha Ndege cha Shinyanga kilichopo kata ya Ibadakuli.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa
mawasiliano Shinyanga mjini mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la mawasiliano Nchini TTCL Peter Ulanga amesema awamu ya
kwanza ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa ulianza Mwaka 2009, ukiwa na uwezo wa 40G
na badae kuongezeka uwezo kuwa 200G.

Ameeleza kuwa katika awamu hii uwezo wa mitambo
umeongezeka kutoka 200G mpaka 800G ambapo tayari mitambo hiyo inafanya kazi kwa
Singida – Shinyanga – Mwanza na Shinyanga – Kahama na kwamba ujenzi bado
unaendelea katika maeneo mengine.

“Awamu
ya kwanza ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa ilianza Mwaka 2009, ikiwa na uwezo wa
40G na badaye kuongezwa uwezo kuwa 200G na badaye kuongezwa uwezo wa 400G kwa
Singida – Shinyanga – Mwanza  ujenzi wa
awamu hii umeanza toka 20212022 maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na Mkoa wa
Shinyanga, ujenzi  wa Mkongo wa Taifa
Mkoani Shinyanga umejikita katika maeneo makuu mawili ambayo ni usimikaji wa
mitambo na ujenzi wa nguzo za zege sambamba na uvutaji wa Waya za Faiba”.

“Katika
awamu hii uwezo wa mitambo umeongezwa kutoka 200G MPAKA 800G na tayari mitambo
inafanyakazi kwa Singida – Shinyanga – Mwanza, na Shinyanga – Kahama na ujenzi
unaendelea maeneo mengine”.
amesema Peter

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya
habari Mhe. Nape Mnauye amesema Wizara hiyo inaendelea kuboresha miundombinu ya
mawasiliano ambapo Mkongo ni moja ya njia ya mawasiliano ya kimtandao.

Duniani
inakwenda kwenye uchumi wa kidigtali uchumi huu unatumia Barabara kubwa na
ndogo lakini zenyewe ziko kwenye ulimwengu wa mtandao na kazi yetu
nikutendeneza miundombinu kwenye ulimwengu wa kimtandao ili watu wawasiliane
wabadilishane bidhaa muuzaji na mnunuzi wakutane kwenye ulimwengu wa kimtandao na
ili wakutane wanahitaji miundombinu ya kimtandao na ndiyo maana tunajenga
Mkongo mkubwa na tunajenga pia na Mikongo midogo lakini pia tunajenga Minara ambayo
yote kwa pamoja lengo lake moja tu kuwafanya watu na taasisi ziweze kuzungumza
ziweze kusomana ziweze kuwasiliana ziweze kufanya biashara  kwahiyo kwa kifupi Mkongo ni Barabara ya
mawasiliano ya kimtandao”.
amesema Waziri Nape

Kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu ikiongozwa
na Mwenyekiti yake  ambaye ni Mbunge wa
jimbo la Mpanda vijijini Mhe. Seleman Moshi Kakoso imeipongeza Wizara ya
habari, mawasiliano na teknolojia ya habari kwa ubunifu huo huku wakiisisitiza
TTCL kuusimamia Mkongo wa Taifa huo ili uweze kujiendesha  kibiashara kwa kuwa unatoa huduma zinazoingiza
Fedha.

“Kamati
ya Bunge ilipambana kuhakikisha TTCL mnaumiliki Mkongo wa Taifa sasa
tunachowaomba mkisimamie msije mkawa mnategemea ile ruzuku ya Serikali sisi
tunataka Mkongo wa Taifa ujiendesha kibiashara kwa sababu mnatoa huduma ambazo
zinaleta Fedha nyingi mnapelekea huduma Burudi, Rwanda, Kenye na kwingineko lakini
pia ndani ya Nchi hum tunaomba mkae ukiwemo wewe Mkurugenzi uhakikishe unakuwa
mbunifu mnausimamia huo Mkongo ili uweze kujiendesha kibiashara”.
amesema
Mhe. Kakoso

Aidha Kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu
wakati ikitembelea na kukagua mradi katika ukarabati na uboreshaji wa kiwanja
cha Ndege cha Shinyanga imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ambao
unatarajiwa kukamilika Oktoba 3,2024.

Katika taarifa yake kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) Dorothy Mtenga amesema hadi sasa mradi
umefikia asilimia 11,02 ambapo tayari umetoa jumla ya ajira 115 kati ya hizo,
ajira 100 sawa na asiliamia 87 zimetolewa kwa watanzania.

Amesema baada ya kukamilika kwa meadi huo
utarahisisha usafiri kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga, Simiyi na mikoa ya jirani
pia utarahisisha shughuli za kibiashara hasa Madini, ufugaji na Kilimo.

Ametaja faida zingine kuwa, mradi huo utarahisisha
shughuli za kijamii, utaguza uchumi wa Mkoa wa Shinyanga na Simiyu lakini pia
utasaidia shughuli za utafiti wa Kilimo pamoja na kusaidia kukuza utalii wa
Mkoa wa Shinyanga Mikoa jirani na Taifa kwa ujumla.

Mhandisi Dorothy ametaja hatua mbalimbali
zilizokamilika katika mradi huo ikiwemo Barabara ya kuruka na kutua Ndege
(Ruwey) asilimia 40.3 pamoja na uhamishaji wa miundombinu ya Maji, Umeme na
mawasiliano kwenye eneo la ujenzi.

“Hadi
sasa mkandarasi amekamilisha kazi ya ujenzi wa ofisi ya Mhandisi mshauri kwa
asilimia mia moja (100), amekamilisha Barabara ya kuruka na kutua Ndege
(Runway) kwa asilimia 40.3, Maegesho (Apron) 
asilimia 40, Barabara ya kiungio (Taxiway) asilimia 40, ujenzi wa
Contactors Camp mitambo ya kufanya kazi asilimia mia moja (100), kusafirisha
eneo la jingo la Abiria asilimia mia moja (100)”.

“Lakini
pia mkandarasi kazi zingine zilizokamilika ni kusafisha eneo la maegesho ya
Magari asilimia mia moja, kusafisha eneo la ujenzi wa uzio asilimia kumi (10)
uchimbaji wa msingi wa jingo la Abiria asilimia mia moja, ujenzi wa msingi wa
jingo la Abiria asilimia 90, ujenzi wa jingo la Abiria asilimia 15, vifaa vya
ujenzi(Materials) asilimia 80, kuagiza vifaa vya uendeshaji wa jingo vyenye
kuchukua asilimia 50 ya maendeleo ya ujenzi ni asilimia 30, ujenzi wa Nguzo
asilimia mia moja, ujenzi wa Tenki la kuhifadhi maji asilimia tano (5), ujenzi
wa eneo la kuegesha Magari asilimia 35 pamoja na ujenzi wa formworks kwa ajili
ya ghorofa ya kwanza umefikia asilimia 45”.
amesema Dorothy

Baada ya kamati ya kuduma ya Bunge ya miundombinu
kutembelea na kukagua mradi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Seleman Moshi
Kakoso ametoa maelekezo mbalimbali ikiwemo suala la CSR pamoja na kuhakikisha
mkandarasi atatekeleza wajibu wake ili kukamilisha mradi kwa wakati.

“Jambo
la kwanza Serikali inawataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo haya mradi huu
uweze kuwanufaisha wapate CSR jambo la pili ni kumsimamia mkandarasi atimize
wajibu wake afanye kazi kwa wakati mradi uendane sambamba na mkataba aliosaini
pamoja na ufanisi wa kazi jambo la mwisho tunamuomba mkandarasi aweze kuwatumia
vijana wa kitanzania kwenye maeneo wanayofanya kazi lakini waweke usawa juu ya
malipo kwahiyo haya yakitekelezwa mradi utaenda vizuri na utaweza kuwasaidia
watanzania”.
amesema Kakoso

Ukarabati wa kiwanja cha Ndege Shinyanga awamu
inayoendelea unafadhiliwa kwa fedha ya mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya
uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB).
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *