Kamati ya wanawake tughe mkoa wa shinyanga yatoa zawadi kupunguza mahitaji kituo cha afya bulungwa halmashauri ya ushetu

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya Wanawake wa Chama cha wafanyakazi wa
serikali na Afya TUGHE Mkoa wa Shinyanga leo imetoa  zawadi ya mahitaji mbalimbali ikiwemo
Kompyuta pamoja na mzani wa kupimia watoto wachanga katika kituo cha Afya
Bulungwa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, ikiwa ni sehemu ya  maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Hafla ya kukabidhi vitu hivyo imefanyika katika  viwanja vya kituo cha Afya Bulungwa ambayo
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali na kwamba mgani rasmi ni Diwani wa kata ya
Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe.
Emmanuel Chelehani.

Akizungumza kaimu Mwenyekiti wa kamati za Wanawake TUGHE
Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally Choyelo amesema kamati  hiyo imekuwa na utaratibu kila Mwaka wa kufanya
matendo ya huruma kwa kutua huduma katika maeneo mbalimbali na kwamba Mwaka huu
wameguswa kupunguza changamoto ya vitendea kazi katika kituo cha Afya Bulungwa.

“Katika
kutekeleza hilo tumeona ni vyema sasa tuje tushirikiane na nyie kama Bulungwa
kama Ushetu ili tuweze kutoa vile tulivyoviandaa kutoka kwa akina Mama wa TUGHE
Mkoa wa Shinyanga jambo hili siyo mara ya kwanza kulifanya Miaka yote tumekuwa
tukijipanga na kutembelea sambamba na kutoa hizi huduma Mwaka jana tumefanya
katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na tulienda kutembelea vituo
mbalimbali kwahiyo dhima kubwa ni katika kutekeleza sera ya TUGHE kama sulogani
yetu inavyosema HUDUMA BORA MASLAHI ZAIDI”.
amesema Bi.
Mariam

Katibu wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga
Catherine Masalu amevitaja vitu hivyo vilivyotolewa na kamati hiyo ya TUGHE Mkoa
wa Shinyanga ikiwemo kitambaa cha kijani kwa ajili ya wazazi na huduma za
upasuaji ambapo amesema kamati hiyo itaendelea kutembelea Halmashauri za Mkoa
wa Shinyanga kufanya matendo ya huruma kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali.

Kama inavyofahamika
kwamba kila ifikapo Machi 8 huwa ni maadhimisho ya siku ya Wanawake na sisi
kupitia chama cha wafanyakazi TUGHE huwa tunafanya matendo ya huruma kwa jamii na
safari hii matendo ya huruma tumeyafanyia katika kituo cha Afya Bulungwa
iliyopo Halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga”

“Katika
kituo hiki tumetoa mahitaji mbalimbali ikiwemo Machine ya kupimia  sukari, Kompyuta mbili (2), Kitambaa cha
kijani kwa ajili ya wazazi na huduma za upasuaji, Mzani  wa kupimia watoto  wachanga pamoja na  Roll 
moja ya green material”.
amesema Bi. Catherine

Mganga mkuu wa Wilaya ya Ushetu Dkt. Athuman Matindo
pamoja na mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bulungwa wemeishukuru kamati hiyo
ya  chama cha TUGHE Mkoa wa Shinyanga, kwa
kuguswa na changamoto za kituo hicho ambapo ameahidi kuvilinda na kuvitumia
kama ilivyokusudiwa katika kurahishisha huduma kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Diwani
wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni Baluhya naye amewapongeza Wanawake
hao kwa majitoleo yao ambapo amesema kuwa ofisi ya Mbunge itatoa mahitaji
mengine katika kituo hicho ndani ya Miezi mitatu.

“Mhe.
Mbunge amenituma kusema Infusion Mashine ataileta ndani ya Miezi mitatu pamoja
na Hormone Analyzer  hizi zitakuja ndani
ya Miezi mitatu kwa hatua hii wana Bulungwa tutakuwa tumevuka malengo ya maombi
yetu, naomba zawadi hizi ni zawadi zilizogharamikiwa kwa gharama kubwa sana
naomba usimamizi wako Mganga mfawidhi wa kituo hiki vifanye kazi lengwa tu, kwa
malengo ya wagonjwa tu na wataalam wako naomba kabisa vipokeeni lakini pia vitunzeni”.
amesema
Mhe. Baluhya

Kwa upande katibu wa TUGHE Mkoa wa Bwana Ramadhan
Pangara amemshukuru mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bulungwa kwa ushirikiano
wake katika kubainisha changamoto zilizopo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wafanyakazi ambao bado hawajajiunga na chama hicho waweze kujiunga ili
kunufaika na fursa mbalimbali.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Ushetu Velena Peter wakati akifunga hafla hiyo ameipongeza kamati ya Wanawake
wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa zawadi hizo huku akiwahakikishia kuendelea
kufuatilia ahadi za ofisi ya Mbunge kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa
changamoto katika kituo cha Afya Bulungwa.

Kamati ya Wanawake wa Chama cha wafanyakazi wa
serikali na Afya TUGHE Mkoa wa Shinyanga Machi 11,2024 imetoa
  zawadi ya mahitaji mbalimbali pamoja na
kutembelea wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Bulungwa Halmashauri ya Wilaya
ya Ushetu, ikiwa ni sehemu ya
 maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa
Shinyanga Bi. Mariam Ally Choyelo akieleza dhima ya kamati hiyo.

Katibu wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga
Catherine Masalu akitaja mahitaji yaliyotolewa na kamati hiyo.

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Bwana Ramadhan Pangara akiwaomba
watumishi wa Afya kujiunga na chama hicho.

Mwenyekiti wa TUGHE Wilaya ya Ushetu Dkt. John Duttu akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani
Mteganoni Baluhya akizungumza kwa  niaba
ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu.

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani
Mteganoni Baluhya akizungumza kwa  niaba
ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu.