Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia legal aid yazinduliwa rasmi shinyanga yatajwa kuwa fursa kwa wananchi

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali mkoani
Shinyanga imesema kampeini ya kitaifa ya msaada wa kisheria ni fursa ya
kupunguza migogoro mbalimbali ya wananchi hasa wasiokuwa na uwezo wa kumudu
gharama.

Akizundua
rasmi kimkoa utekelezaji wa Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria iliyopewa
jina la Mama Samia Legal Aid (MSLAC)
mgeni rasmi, mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme amesema kampeni hiyo ni fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Amesema kupitia kampeni hiyo wananchi watapata fursa
ya kujengewa uelewa katika masuala mbalimbali ikiwemo kutambua haki na wajibu
wa misingi ya utawala bora.

RC Mhe.Mndeme amesema ili wananchi wa Shinyanga waweze
kunufaika na kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria huduma hiyo itatolewa
bure hivyo wananchi wanapaswa kutumia fursa hiyo.

Ametoa wito
kwa wananchi Mkoani Shinyanga kutumia nafasi hiyo  kupata huduma ya msaada wa kisheria bure
kupitia kampeini hiyo ambayo inaanza leo na kwamba
lengo
la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii

“Kupitia
kampeni hii msaada wa kisheria utatolewa bure katika Halmashauri 6 zote za Mkoa
wa Shinyanga kuanzia leo Tarehe 11 mwezi wa sita mpaka tarehe 21 mwezi wa sita
Mwaka huu 2023 wananchi wote mnaalikwa kushirikia kupata huduma hizi ambazo
zitatolewa katika Halmashauri zetu jitokezeni kwa wingi kampeni hii ni bure
wote mtahudumiwa kwa usawa usitoe hata shilingi moja”.
amesema
RC Mndeme

Aidha mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameliagiza jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga kushughulikia haraka iwezekanavyo kesi zote zinazohusu ukatili wa
kijinsia, ambazo zimekaa muda mrefu kusubiri upelelezi.

Amesema kuwa,
watuhumiwa wa kesi hizo ikiwemo zinazohusu ndoa, mimba za utotoni na ubakaji
wanapaswa kupatikana haraka na kufikishwa Mahakamani ili hatua zaidi ziweze
kuchuliwa.

Mhe. Mndeme
amebainisha kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan ameasisi kampeni hiyo ili kuondoa viashiria vyote vya kuminya
upatikanaji wa haki, hususani vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto
ambavyo ndiyo changamoto kubwa katika mkoa wa Shinyanga.

RC Mndeme
amewataka wakuu wote wa Wilaya zilizopo katika mkoa wa Shinyanga kwenda
kusimamia kwa karibu utekelezaji wa kampeni hiyo na kuwashirikisha viongozi wa
ngazi zote wakiwemo Wenyeviti wa Vjiji na vitongoji, watendaji wa Kata na
Vijiji, Makatibu tarafa na viongozi wa vyama vya siasa pamoja na kuhakikisha
kila kata inayohusika na kampeni hiyo inatenga chumba maalum kwa ajili ya
wasaidizi wa kisheria .

Akizungumza
naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul, amesema Serikali
inaendelea kuboresha mifumo ya haki jinai katika maeneo mbalimbali ya Nchi,
ikiwemo kujenga ofisi ya Mwendesha mashtaka katika mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya katiba na sheria
Mary Makondo amesema kampeni hiyo itawasaidia wananchi waliowengi hasa
wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili.

Naye Meneja rasilimali na mawasiliano wa shirika la
Legal Services Facilty (LSF)  Bi. Jane
Matinde pamoja na mambo mengine amesema kampeni hiyo itakomesha vitendo vya
ukatili.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria
ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada
wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija ametaja baadhi ya mapendekezo
ambayo yamelenga kufanikisha kampeni hiyo ikiwemo
 kutungwa kwa sheria mahususi ya kupinga
ukatili, pamoja na kufanyiwa marekebisho kwa sheria zinazowakandamiza wanawake.

Mwenyekiti
huyo ameiomba Serikali kuwa na mfumo maalum wa kuwawezesha wasaidizi wa
kisheria, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Tunapendekeza kuwa na madawati ya
malalamiko kwenye ofisi za wakuu wa Wilaya na wawepo wasaidizi wa  kisheria 
kwa ajili ya kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi, kwa
kutambua ukatili wa kijinsia ni kikwazo katika kuwezesha wananchi kufikia haki
kwa wakati ni pendekezo letu kuwa serikali ilidhie kutungwa kwa sheria ya
kupinga ukatili wa kijinsia Tanzania na marekebisho ya sheria mbalimbali
zikiwemo zinazosababisha ukatili wakijinsia hususan ni kwa wanawake katika
sheria ya ndoa na miradhi ambazo bado ni changamoto kwa kwenye jamii”.
amesema Bwana Shija

Nao wabunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mzava  na Mhe. Santiel Kirumba  wamesema watashirikia kikamilifu katika
kuhakikisha huduma ya msaada wa kisheria inawafikia wananchi ili kupunguza migogoro
ikiwemo ya Ndoa, Ardhi pamoja na ukatili.
Bottom of Form

Kampeni ya kitaifa
ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid imelenga kutoa msaada wa kisheria
kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni na wale wasiokuwa na uwezo, ambapo itadumu
kwa takribani miaka mitatu kuanzia mwaka huu.

Kampeni hiyo  imezinduliwa leo Juni 11,2023 ambapo huduma
hiyo itatolewa bure na kwamba inakwenda na kauli mbio inayosema msaada wa
kisheria kwa haki, usawa, amani na maendeleo.

Uzinduzi wa
Kampeni hiyo kimkoa ambao umefanyika leo katika uwanja wa Sabasaba Kambarage
mjini Shinyanga, umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma za
msaada wa kisheria, wawakilishi wa taasisi na Mashirika mbalimbali ya Serikali
na yasiyokuwa ya Kiserikali pamoja na wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akizindua Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Naibu Waziri
wa Katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul
akizungumza
kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya
Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo
Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Mary Makondo akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Meneja rasilimali na mawasiliano wa shirika la Legal
Services Facilty (LSF)  Bi. Jane Matinde akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria
ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada
wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akizungumza
kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya
Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo
Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Mwenyekiti wa uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria
ya  Mama Samia  ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya msaada
wa kisheria Mkoa wa Shinyanga Bwana John Shija akizungumza
kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya
Msaada wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo
Jumapili Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Shinyanga Dkt. Christina Mzava
akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Shinyanga
Mhe. Santiel Kirumba   akizungumza kwenye uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Bwana Donald Magesa
akizungumza kwenye
uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Msaada
wa Kisheria inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili
Juni 11,2023 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
.

Hafla ya uzinduzi   Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria
inayojulikana kwa jina Mama Samia Legal Aid Campaign leo Jumapili Juni 11,2023
katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga
ikiendelea.