Kangi lugola kuhojiwa na takukuru kesho

Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola anatarajiwa kuhojiwa kesho na
Taasisi ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

 Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema
walianza kukusanya taarifa za awali ambazo zimeshakamilika na wahusika
wote wataitwa kesho kuhojiwa.

Rais
Dkt John Magufuli alitengua uwaziri wa Lugola kutokana na tuhuma za
utiaji saini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya Zimamoto na
Uokoaji vyenye thamani ya Euro Mil. 408.2 kutoka kampuni moja ya nje ya
nchi.