Kanyasu aitaka kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa tabora kuchukua hatua dhidi ya viongozi kisiasa wanaochochea wafugaji kuwavamia watumishi wa maliasili

Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameitaka Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora kuwachukulia hatua wanasiasa na watu ambao
wamekuwa wakiwachochea wafugaji kuingia katika maeneo ambayo yamezuiliwa
na kuwavamia na kuwashambulia Askari ya Wanyama pori wanapokuwa
wakitekeleza majukumu yao.Alisema
hatua imesababisha kuwawa kwa Asakari wawili katika eneo la misitu ya
Isawima wakati walipokuwa wakijaribu kuwaondoa katika misti hiyo hivi
karibuni.

Kanyasu
alitoa kauli hiyo leo Mkoani Tabora wakati akizungumza na wafanyakazi
wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya wa Maliasili na Utalii na uongozi
wa Mkoa wa Tabora.

Alisema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa mgogoro wa Mistu ya Hifadhi wa Isawima
umekuwa ukichochewa na Kiongozi wa Wafugaji ambaye pia ni Kiongozi wa
Kisiasa katika eneo la hilo wilayani Kaliua, jambo linasababisha Askari
kuvamiwa na kuwawa.

Kanyasu
alisema ni vema hatua dhidi ya Kiongozi huyo zikachukuliwa kwa ajili ya
kuwafanya watumishi wa Wizara ya Maliasi na Utalii na wengine ambao
wanashughulika kulinda maeneo ambayo yamehifadhiwa kufanya kazi katika
mazingira salama.

Aidha
alisema watu wanaoendesha uvamizi na mauaji ya watumishi wanalinda
maeneo yaliyozuiliwa  wanajulikana kwa kuwa wanamiliki ng’ombe , hivyo
ni vema wakatafutwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili maamuzi
yajulikane kwa watu hao.

Kanyasu
alisema vitendo hivyo visipochukuliwa hatua kali wavamilizi wataendelea
kutekeleza mauaji na kuona kuwa wao wako sahihi kuendelea kuharibu
maliasili na kuhatarisha maisha ya wanyamapori na wananchi wanaotegemea
mistu hiyo kupata maji.

“Anapowawa
mtumishi analinda maeneo yaliyozuiliwa hakuna mtu anayepiga kelele
..lakini wavamizi wanapoondolewa na vibanda vyao kuchomwa moto
wanajitokeza watu kuwatetea na kupiga kelele…inasikitisha sana” alisema.

Kwa
upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema tatizo
hilo limeshaundiwa Kamati ya Uchunguzi na wanatarajia kutoa majibu ya
kilichobainika na hatua za kuwachukulia wahusika hivi karibuni.

Katika
hatua Naibu Waziri huyo aliwaonya watu ambao wametafisiri vibaya tamko
la  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania la kuruhusu vijiji 900
vilivyo kwenye hifadhi kuwapati hati na wao kuanza kuvamia maeneo
mengine mapya kuwa watachukuliwa hatua kali.

Alisema
tamko la Rais Magufuli halikusema kuwa watu waanze upya kuingia katika
maeneo mapya kwa mtanzamo kuwa ipo siku nao wataruhusiwa kuendelea na
shughuli zao.

Kanyasu alisema watakaokutwa katika maeneo ambayo yamezuiliwa watachukuliwa hatua kama wavamizi.