Katibu mkuu adc doyo atoa ushauri kwa rais samia


Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) Doyo Hassan Doyo akizungumza katika kikao chake na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani kwenye uchaguzi mkuu uliopita alipokutana nao Jijini Tanga ikiwemo kuweka mikakati ya kujiimarisha zaidi kuelekea kwenye chaguzi zijazo

Katibu mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change
(ADC) Doyo Hassan Doyo akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho

Katibu mkuu wa Chama cha Alliance Democratic Change
(ADC) Doyo Hassan Doyo amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Serikali inapitia upya na
kuziangalia tena kesi za uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha na kesi
za ugaidi ambazo zinawakabili baadhi ya watanzania wanaoteseka
magerezani kwa muda mrefu bila kupatikana ufumbuzi wake.
Hatua
hiyo ya Katibu mkuu huyo inatokana na namna ambavyo Rais Samia
alivyoonesha dhamira ya kupambana haki na wajibu basi aangalie vizuri
sheria na ziweze kufanyiwa marekebisho lakini pia waliokamatwa na
kuwekwa magerezani serikali iangalie namna ya kuzifuta kesi hizo ili
watanzania waweze kunufaika na matunda ya nchi yao. 
Katibu
Mkuu huyo alisema kwasababu watanzania wengi wanateseka kutokana na
kesi walizopewa za uhujumu uchumi,  utakatishaji wa fedha na kesi za
ugaidi kutokuwa na dhamana inapelekea watanzania wengi kuendelea
kuteseka. 
Alisema kwa
sababu Rais ameonyesha dhamira ya kupambana na kesi za namna hiyo basi
kesi za namna hiyo ziangaliwe upya na ziweze kufutwa. 
“Watanzania
wenzetu wanaendelea kuteseka na kesi hizo ambazo hazina dhamana
kwasababu Rais ameonyesha nia ya kupambana basi aangalie namna ya
kubadilisha hizi sheria zinazowakandamiza watanzania wenzetu kwanini
tunatoa ushauri huu kwasababu tumemsikia Rais mwenyewe akisema kwamba
Takukuru wamefuta kesi zaidi ya 140 za kubambikiza, “
Aliongeza
kuwa hata hizi karibuni alipokuwa akifungua kiwanda cha polisi cha
kushonea yunifomu akasema na  nyie jeshi la polisi angalieni angalieni
kama kuna kesi za kubambika na nyie mzifute kwa kauli ya Rais ni
mategemeo yetu kwamba hata hizi kesi zinazoitwa za uhujumu uchimi ,
utakatishaji wa fedha na kesi za ugaidi pengine nazo ni za kubambikiza.
Alisisitiza Doyo. 
Alisema
chama hicho wanaishauri Serikali kupitia Rais msikivu Samia Suluhu
Hassan  kwenye majukumu na maamuzi mazito aweze kuwafikiria watanzania
ili waweze kuishi nao kwa amani kama watu wengine wanavyoishi. 
“Unapopewa
kesi ya uhujumu uchumi , utakatishaji wa fedha na kesi ya ugaidi kwa
mujibu wa sheria zetu hazina dhamana na kitendo cha kumzuia mtu dhamana
maana yake umwmnyima haki yake ya kikatiba ya msingi hivyo tunaomba
sheria hizi ziweze kuangaliwa upya ili watanzania waweze kunufaika na
matunda ya nchi yao.,”alisema Katibu Doyo. 
Awali
akizungumzia dhamira ya ziara yake nchi nzima Katibu Doyo alisema ni
kukutana na wanachama wao kuwapa pongezi kwa wale walioonyesha nia ya
kuwania, nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu uliopita na kuwapa pole
kwa kimbunga walichokutana nacho katika uchaguzi huo lakini pia kuweka
mikakati ya pamoja kuelekea kwenye uchaguzi wa serijali za mitaa. 
 

“Dhamaira
ya kwanza ni kuja kutathimini kipigo cha uchaguzi mkuu uliopita lakini
sasa tunajipanga kuelekea uchaguzi wa 2025 kwakuwa Rais aliyepo amesema
uchaguzi ujao atakayepata amepata na atakayekosa amekosa ni tofauti na
Rais aliyepita hivyo tulivyopata matumaini ya, mheshimiwa Rais sisi kama
chama tumeona tuchukue hatua za kuweza kukutana na nyinyi kuwapongeza, 
kuwapa pole lakini sasa tujipange na uchaguzi ujao tukiwa na matumaini
ya kufanya vizuri, “alibainisha Doyo. 

Katibu
Doyo alisema ameanza ziara tarehe 2 katika jiji la Daresalaam na wilaya
zake zote,   Unguja na Pemba,  pamoja na Tanga ya kuongea na viongozi
pamoja na watendaji na kubainisha kuwa ziara hiyo ni ya nchi nzima
ambapo anaelekea Morogoro,  Singida, Dodoma,  Mwanza, Mara Simiyu, 
Geita,  na Kigoma na mara baada ya hapo mapumziko mwezi ujao tarehe 15
wataendelea na ziara mikoa ya kusini kwa kusudio la kuinua uhai wa
chama.