Kauli kangi lugola baada ya rais magufuli kumtumbua na kusema hafai

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema ataendelea kumsaidia Rais  Magufuli   kwa kuwa yeye ni mbunge wa Mwibara (CCM).


Lugola
ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 23, 2020  jijini Dar es Salaam
muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya uzinduzi wa nyumba za  maofisa
wa Jeshi la Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Alieleza
hayo baada ya Rais  Magufuli  ambaye wakati akizungumza  katika
uzinduzi huo kusema Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Thobias  Andengenye hawafai kuendelea na nyadhifa zao kutokana
na mambo waliyoyafanya kuhusu uingiaji wa mikataba.

“Rais
ndiye aliniteua kwenye Baraza la Mawaziri na ndiye ameona anipumzishe,
kwangu mimi ni jambo la faraja, Watanzania mmemsikia Rais hatua
aliyochukua ni hatua nzuri na inalenga kujenga safu ya Serikali,
ninaahidi kama Mbunge ambaye nilipata nafasi ya kumsaidia Rais
nitaendelea kumsadia kwa kwa heshima kubwa.” Amesema Lugola