Dawa za mitishamba zikiwa tayari kutumiwa |
majani ya aina mbalimbali za miti iliyokuwa ikitumiwa kujifukizia wakati wa ugonjwa wa corona |
Mganga wa tiba asili akiwa na dawa zake za asili pembeni |
-WATINGA KWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI KUTHIBISHA DAWA YA CORONA
-WATAMBA WALIIWEZA ‘SURUA’ CORONA INATIBIKA BILA TATIZO
Na
Mwandishi Wetu, Arusha
AGIZO
alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli la
kutaka dawa za asili zianze kuruhusiwa kuuzwa nchini, limeanza kuzaa matunda
baada ya waganga wa jadi na tiba za
asili kuanza usajili wa dawa zao.
Wakizungumza
juzi jijini hapa wakiwa katika harakati za kutafuta usajili wa dawa zao, katika
maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kanda ya kaskazini, baadhi ya waganga wa
tiba za asili kutoka maeneo mbalimbali kanda ya kaskazini walipongeza maamuzi
ya Rais Dkt.Magufuli ya kuruhusu matumizi ya dawa zao.
Hata
hivyo alisema kauli hiyo imechelewa kwa kuwa ni miaka mingi wao kama waganga wa
tiba za asili wamekuwa wakitibia wagonjwa kwa kutumia dawa za asili za mizizi,
majani na matunda na wagonjwa kupona.
Walisema
kuwa ugonjwa wa corona (Covid -19), ambao umeendelea kuua maelfu ya watu
duniani, dawa yake ipo miongoni mwa dawa ambazo wamekuwa wakizitumia kutibia
wagonjwa wao na kwamba kupitia dawa hizo wagonjwa waliogundulika nchini
waliweza kupona.
“Tunamshukuru
sana Rais Dkt Magufuli kwa kutambua umuhimu na ubora wa dawa za asili, wakati
janga la Corona lilivyoingia alisimama kidete na kutoa msimamo dhabiti kuhusu
matumizi ya dawa za asili kwa kunywa na kujifukiza, na kweli tulipona,”alisema
Dkt Daudi Nyaki, Mkurugenzi mkuu wa Chama
waganga wa tiba asili nchini (CHAWATIATA).
Rais
Dkt John Pombe Magufuli akizindua bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu 2020, na yeye kuibuka
mshindi aliziagiza mamlaka husika za dawa kuweka utaratibu wa dawa za asili
kuanza kuruhusiwa rasmi nchini kama dawa zinazoweza kutibu magonjwa mbalimbali
baada ya kufanyia uchunguzi na kuthibitishwa.
Kwa
mujibu wa Dkt Nyaki baada ya kusikia tangazo la Mheshimiwa Rais baadhi ya waganga
wa tiba asili kupitia chama chao walijikusanya na kukusanya dawa za asili
ambazo wanaamini zinatibia ugonjwa wa Corona na kupeleka kwa mkemia mkuu wa
Serikali.
Mkurugenzi
mkuu wa Chama hicho,Cha Chawatiata (T) Daud Nyaki,anasema dawa hizo
wamezipeleka kwa mkemia mkuu wa serikali ili kujiridhisha na kuona kiwango cha
ubora wake na uwezo wa kutibu kwa sababu ni mkusanyiko na mchanganyiko wa miti
mbalimbali .
Anasema
wataalamu hao wamekubaliana kupitia Chama chao kwamba kila mtaalam wa tiba
asili awasilishe dawa zake kabla ya kuzitumia ili kuepuka madhara yanayoweza
kujitokeza jambo ambalo wasingependa kuliona.
“
Baada ya kusikia tangazo la Rais kila mmoja alichuma majani, kuchimba mizizi ya
miti na magome yake na kisha kutoka na mzigo wa kutosha ambao wanaamini kuwa ni
tiba tosha ya ugonjwa wa Corona, na hakika tiba hii ni sahihi kabisa, tunaamini
mkemia ataturejeshea majibu mazuri,”alisema.
Alisema
kuwa mlipuko wa magonjwa kama hayo umekuwepo mara kwa mara ulimwenguni na kwa
nyakati tofauti wataalam wa tiba asili wamekuwa wakitumika kutafuta tiba
na wamekuwa wakifanikiwa.
“Mfano
ugonjwa wa surua ulipoingia duniani watu wengi sana walikufa kwa kuwa ulikosa
tiba lakini kupitia mizizi yetu ya asili, tuliweza kuokoa watu wengi kwa
kujifukiza na kunywa dawa za asili, hata corona na yenyewe mwanzo ilileta
taharuki kubwa sana, lakini dawa zetu za asili zilikomesha kabisa,”alisema.
Alisema
mbali ya kutafuta uhakiki wa ubora wa dawa hizo kwa mkemia mkuu wa Serikali pia
baada ya kupata uhakika wa tiba zake pia itakuwa ni kuziongezea thamani na
hivyo kuondoa dawa ambazo ni sumu na zinazoweza kuleta athari kwa afya ya mtumiaji.
Ugonjwa
wa Corona umekuwa ni tishio kubwa sana ulimwenguni lakini nchini imekuwa ni
tofauti baada ya Rais Dkt Magufuli kuruhusu tiba za asili kutumika mara baada
tu ya kugundulika kuingia nchini na matokeo yake yaliweza kusaidia kupungua kwa
vifo na kupotea kwa ugonjwa huo.