Kesi ya kutekwa mfanyabiashara mohammed dewji yapigwa kalenda hadi january 21

Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imepiga kalenda kesi ya
kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu kama MO inayomkabili
dereva wa taksi Mousa Twaleb na wenzake wanne ambao bado hawajakamatwa
na kufikishwa mahakamani hapo.


Kesi
hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu
baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aliyepangiwa kusikiliza kesi
hiyo kwenda likizo.

Wakili
wa Serikali, Faraji Nguka, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya
kutajwa.

Hakimu Chaungu alisema kesi hiyo itatajwa Januari 21, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.

Watuhumiwa
wengine ambao upande wa mashtaka inawatafuta ni raia wanne wa Msumbiji
na mmoja wa Afrika Kusini, wanaodaiwa kumteka bilionea huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *