Kifo cha mwenyekiti wa kijiji cha mtoa machozi mbunge elibariki kingu

 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu, akilia wakati wa dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba 22 mwaka huu nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida.


 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu (katikati) akishiriki dua hiyo.
 Katibu wa Msikiti Mkuu Kata ya Sepuka, Juma Mwango akizungumza kwa huzuni.
 Mmoja wa wanafamilia ya marehemu, Ahmed Shabani akilia kabla ya kuanza kwa dua hiyo.
 Vijana wakilia.
 Ni  vilio.
 Ni huzuni tu
 Wazee wakiwa na huzuni wakati wa dua hiyo
 Mwalimu wa Msikiti wa Mtunduruni mjini Singida, Hamisi Ndida akizungumza.
 Wakina mama wakiwa kwenye dua hiyo.
 Ni huzuni tupu.
 Diwani Mstaafu wa Kata hiyo, Juma Ntandu akizungumza.
 Vijana wakiwa wamebeba chakula kwa ajili ya dua hiyo.
Waombolezaji
wakiwa kwenye dua ya kumuombea Mzee Jumanne Njoghomi aliyefariki Oktoba
22 nyumbani kwake Kata ya Sepuka mkoani Singida. Marehemu enzi za uhai
wake alikuwa ni  aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Musini
Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka 15.
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
KIFO
cha Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji Cha Musini na Mjumbe wa Kamati ya
Siasa Kata ya Sepuka Mkoani Singida,  Mzee Jumanne Njoghomi kimeleta
simanzi kubwa kwa watu waliokuwa wakimfahamu na kumtoa machozi Mbunge wa
Singida Magharibi Elibariki Kingu wakati wa kumuombea dua marehemu.
 
Wengine
walioshindwa kujizuia na kuanza kulia kufuatia kifo cha mwenyekiti huyo
ni pamoja na wazee,vijana,wanawake na hali hiyo imetokana na uchapaji
kazi, ukarimu na upendo aliokuwa nao kiongozi huyo kwa wananchi.
 
Mbunge
Kingu akimuongelea marehemu katika dua hiyo iliyofanyika mwishoni mwa
wiki alisema kifo chake kimewagusa watu wengi pamoja na yeye kwani
alikuwa ni mshauri wake kwa mambo mengi.
 
“Huyu
mzee kwangu alikuwa ni baba na mshauri wangu kwa kweli nimepata pigo
sana nashindwa namna ya kumzungumzia” alisema Kingu huku akitokwa
machozi.
 
Mkazi
wa kata hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lissu alisema hakika
kila mtu atavuna alichokipanda akiwa hapa duniani kwani mzee Njoghomi
alipanda mema na yameonekana baada ya kifo chake hivyo watu tuliopo baki
duniani hatuna budi kujichunguza na kubadilika kwa kutenda mema ya
kumpendeza mwenyezi mungu.
 
Ahmed
Shabani akizungumza katika dua hiyo alisema ni wakati wa kila mtu
kubadilika na  kuachana na vitendo vinavyomchukiza mwenyezi mungu kama
kugombea ardhi,uchoyo,wizi,dhuluma na kujivuna kutokana na utajiri na
kueleza kuwa vyote hivyo tutaviacha hapa duniani.
 
Mwalimu
wa Msikiti wa Mtunduruni uliopo Singida mjini, Hamis Ndiba alisema
alichopanda marehemu enzi za uhai wake ndicho kinachojidhihirisha baada
ya kifo chake kwani alikuwa mnyenyekevu kwa watu wote na msuluhishi wa
migogoro mbalimbali katika mkoa huo.
 

Marehemu enzi za uhai wake hakumbagua mtu awe mkristo au muislam
aliwasikiliza na kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kuwajulia hali wagonjwa
na kuhudhuria misibani hakika tumempoteza mtu ambaye alikuwa muhimu sana
kwetu” alisema Ndiba.
 
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Sepuka, Juma Mghenyi alisema
marehemu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha
Musini Magharibi kwa miaka 15 na mwenyekiti wa Kijiji cha Musini miaka
15 na mpaka anafikwa na mauti alikuwa ni mjumbe wa kamati ya siasa wa
kata hiyo.
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *