Kijana aliyemtishia mwenzake kwa bastola yamkuta mazito….igp amtaka ajisalimishe polisi

Inspekta
Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka kijana
aliyemtishia mwenzake bastola kuripoti polisi baada ya kuonekana
akifanya kitendo hicho katika picha za video zinazosambaa katika
mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.


Mbali na kuripoti, Sirro amesema anatakiwa kusalimisha silaha yake.

Ametoa
kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa
habari baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga
kukomesha rushwa barabarani.

Sirro
amesema ameagiza kukamatwa kwa kijana huyo lakini amekuwa akipiga
chenga,  amemtaka akajisalimishe mwenyewe kituo cha polisi na kufikishwa
mahakamani.