Kijana mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa mtaa wa sanjo kata ya chamaguha manispaa ya shinyanga ajinyonga hadi kufa kwa kutumia pazia

Baba mzazi

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kijana anayefahamika kwa jina
la Mbogo Sospeter mwenye umri wa Miaka 35 mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya
Chamaguha Manispaa ya Shinyanga amejinyonga hadi kufa kwa kutumia pazia.

Akizungumza Baba mzazi wa
kijana huyo, Mzee Sospeter Makula amesema tukio hilo limetokea  Oktoba 21.2023 majira ya saa mbili usiku baada
ya kijana huyo kutoka kwenye shughuli zake za kila siku.

Mzee huyo ameeleza kuwa
marehemu Mbongo hakuwa na changamoto yoyote ile na kwamba walikuwa wanaishi kwa
amani na upendo.

“Majira
ya saa mbili usiku alikuja kijana wangu akiwa na bodaboda akaniambia nipe
shilingi elfu moja nimlipe huyu bodaboda niliingia ndani nikatoa hela nikampa
huyo bodaboda akaondoka baada ya hapo nilimuacha nyumbani mimi nikatoka
nikaenda kukaa nyumba ya pili tukani kwa jirani yetu baada ya kurudi nyumbani
nilikuta taa ya nje inawaka ila taa ya ndani imezimwa nikaingia ndani kuwasha
ile taa nikamkuta motto wangu amejinyonga na tayari ameshakufa nilihangaika
kuikata ile kamba badaye nikafata kisu nilipoikata kamba basi nikaondoka kwenye
kutoa taarifa kwa majirani”.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo
kata ya Chamaguha Bwana Moshi Ngoyeji amesema baada ya kupokea taarifa za tukio
hilo  alichukua hatua za haraka kutoa
taarifa kwa mamlaka nyingine ikiwemo Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake kamanda wa
jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema  jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili
kubaini chanzo cha tukio hilo.

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha Bwana Moshi Ngoyeji