Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kikundi
Cha Kwaya Ya Bunge kimeaanza Rasmi Kuongoza Kuimba Wimbo Wa Jumuiya
Ya Afrika Mashariki Na Wimbo Wa Taifa Pindi Shughuli Za Bunge
Zinapoanza.

Awali,
wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi na
ufungaji wa mikutano ya Bunge ulikuwa ukiimbwa na kwaya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), lakini leo uliimbwa na watumishi wa Bunge.

Akizungumza
leo Jan,28,2020, bungeni jijini Dodoma Spika Wabunge wa bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema mamlaka
aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuanzia sasa bunge ameliamuru kuwa na desturi ya kuimba nyimbo hizo
muhimu pindi vikao na shughuli za bunge zinapoanza .

Ndugai
amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwafundisha watumishi hao ambapo
baada ya kuimba wabunge waliwapigia makofi kuwapongeza.

___________________
WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
1. Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.