Klabu ya maadili yazinduliwa rasmi shinyanga serikali yazielekeza shule na vyuo kuanzisha klabu za maadili kwa wanafunzi

Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Serikali ya Mkoa wa
Shinyanga imezielekeza  shule na vyuo
Mkoani hapa kuanzisha klabu za maadili kwa wanafunzi ili kuendelea kulinda na
kuimarisha uadilifu kwa wanafunzi na jamii.

Maelekezo hayo
yametolewa leo Jumatatu Oktoba 23,2023 na 
kaimu katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Makana akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
klabu ya maadili Mkoa wa Shinyanga.

Amesema ni muhimu shule
na vyuo Mkoani Shinyanga kuwa na klabu za maadili ili wanafunzi waweze
kujifunza misingi  yenye maadili bora
itakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku.

“Kutokana
na umuhimu wa klabu hii katika kukuza maadili ya watanzania nazielekeza shule
na vyuo vyote Mkoani Shinyanga kuanzisha klabu za maadili za wanafunzi na
wanachuo ili kuwe na wanafunzi waadilifu”.

“Aidha
mratibu wa maadili Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kufanya ufuatiliaji wa klabu
hizo ngazi zote za shule na vyuo ili kuona zinafanyakazi kama ilivyokusudiwa na
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuwa kunauhusiano mkubwa kati
ya wanafunzi wenye maadili mema na kuongeza ufaulu katika masomo yao”.amesema
Makana

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi (Simiyu, Shinyanga na Tabora) Bwana Gerald Mwaitebele amewasisitiza walimu kuwa na utaratibu wa wanafunzi wa klabu za maadili kutoa elimu ya maadili kwenye vikao vya wazazi shuleni.

“Kuna
wazazi wengine ni changamoto kwa sababu ya kukosa uelewa lakini mnavikao vya
wazazi shuleni sasa kabla ya kikao hakijaendelea wale watoto wanakuwa wameandaa
ujumbe kupitia kwenye shairi au ngonjela kwahiyo katika vikao vya wazazi
hakikisha klabu ya maadili inatoa elimu na wazazi wanapata maana wengine
wanafanya kwakutokujua kwahiyo ni muhimu wapate elimu waweze kubadilika”.amesema
Mwaitembele

Kwa upande wake afisa
maadili kanda ya magharibi Onesmo Msalangu amesema klabu ya maadili ni kikundi
au vikundi vya wanafunzi ndani ya shule au vyuo vyenye jukumu la kuratibu na
kufanikisha shughuli za kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha jamii masuala
ya maadili kwa ujumla.

Amesema lengo la klabu
ya maadili nikuwajengea wanafunzi na wanavyuo misingi bora ya maadili tangu
wakiwa shule na vyuoni ili kutengeneza Taifa la vijana waadilifu.

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga
Bakari Kasinyo amesema  mambo yenye
kudumisha uzalengo ni pamoja na kudumisha amani, kuipenda na kuiheshimu jamii,
kuwa mwadilifu, kuwajibika, kujipenda na kuwapenda wengine, kudumisha
demokrasia, kulinda rasilimali zetu, kutunza mazingira, kutii sheria,
kuzingatia haki za binadamu zenye kujenga maadili pamoja na kuchukia kutoa au
kupokea rushwa.

Baadhi ya washiriki
katika hafla hiyo wamewashukuru wawezeshaji wa elimu hiyo huku wakiahidi kwenda
kutekeleza miongozi ya klabu ya maadili ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na
serikali.

Klabu ya maadili leo
imezinduliwa rasmi Mkoa wa Shinyanga ambapo viongozi wametembelea  na kukagua klabu za maadili kwa wanafunzi
katika shule ya sekondari Uhuru pamoja na shule ya msingi Town zilizopo
Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Makana akizungumza wakati akifungua mafunzo
hayo ya klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi
wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele  akizungumza kwenye  mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa
Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi
wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele  akizungumza kwenye  mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa
Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akitoa mada ya
uzalendo kwenye  mafunzo hayo ya klabu za
maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Afisa maadili kanda ya magharibi Onesmo Msalangu akitoa
mada ya mwongozo wa klabu za maadili kwenye  mafunzo hayo Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu
Oktoba 23,2023.

Walimu wa walezi wa klabu za maadili shule za
msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika mafunzo hay
oleo Jumatatu Oktoba 23,2023

msingi, sekondari na vyuo Manispaa ya  Shinyanga wakipongeza na kushukuru kwa hatua
zilizofikiwa na klabu ya maadili.

Viongozi pamoja na washiriki wa mafunzo hayo
wakiwemo Walimu wa walezi wa klabu za maadili shule za msingi, sekondari na
vyuo Manispaa ya  Shinyanga wakiwa katika
picha ya pamoja leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Viongozi wa klabu ya maadili wakitazama igizo
kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru baada ya kuwatembelea kwa
lengo la kukagua klabu ya maadili kwa wanafunzi katika shule hiyo leo Jumatatu
Oktoba 23,2023.

Wanafunzi wa shule ya
sekondari Uhuru 

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bakari
Kasinyo akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru leo
Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald
Mwaitebele akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru
leo Jumatatu Oktoba 23,2023

Katibu msaidizi
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald
Mwaitebele akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru
leo Jumatatu Oktoba 23,2023