Maagizo ya dc mtatiro kwa halmashauri ya manispaa ya shinyanga na tarura kuhusu madai ya fidia kwa wananchi ibadakuli

 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akitoa ufafanuzi na maelekezo katika kero na malalamiko yaliyozungumzwa na wakazi wa tarafa ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga

TAZAMA VIDEO YOTE WANANCHI WAKILALAMIKA DC MTATIRO AKIJIBU

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili
Julius Mtatiro ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwenda kuweka
kambi maalum kwa ajili ya kushughulikia kero za wananchi wanaodai kukosa haki
zao katika tathimini iliyofanyika kwenye makazi ya maeneo yao katika uwanja wa Ndege
wa Mkoa wa Shinyanga uliopo kata ya Ibadakuli.

DC Mtatiro ametoa maagizo hayo  Aprili 5,2024 kwenye mkutano wake wa hadhara, baada
ya kusikiliza na kupokea kero na malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi
wakazi wa tarafa ya Ibadakuli.

 Baadhi ya wananchi hao wamelalamika kukosa
haki yao stahiki katika maeneo waliyokuwa wanaishi na kufanya shughuli zao za
kila siku ambapo kwa sasa eneo hilo limechukuliwa na serikali kwa ajili ya
ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Shinyanga.

Wamesema fedha ya fidia inayotolewa
na serikali haiendani na ukumbwa wa maeneo yao ambapo wamesema tathimini
iliyofanyika katika maeneo yao haikuzingatia utaratibu ulioweka na serikali.

Mmoja wa wananchi aliyelalamika
katika mkutano huo wa hadhara ni Joyce Bala Lukale ambaye amesema amepewa fidia
ya fedha shilingi laki nne kwenye eneo lake ya hekari saba.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili
Julius Mtatiro pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuitaka Halmashauri
ya Manispaa ya Shinyanga kwenda kushughulikia changamoto ya malalamiko ya
wananchi hao ili waweze kupata haki zao stahiki.

“Suala
la fidia na tathimini nadhani kwamba linashida tathimini inapofanywa  mahali inakamilika Halmashauri ya Manispaa zinahusika
moja kwa moja asilimia mia moja kwa nini zinahusishwa Halmashauri kwa sababu ni
serikali za mitaa ninachotaka kuzungumza ni kwamba sisi kwa upande wa serikali
tujipange wanaishi wanaeleza unajua kabisa hajatendewa haki, mtu anahekari aba za
maeneo ana mazao kwenye maeneo ana miti halafu eti anakuja anapewa fidia ya
laki nne siyo tathimini hiyo hii ni felia na watumishi wa serikali tusikubali
hii felia maana tathimini ni haki ya mtu”.

“Kwahiyo
mimi nasema pamoja na kwamba tunaendelea kupambana kutatua hizo changamoto lakini
Halmashauri mjue mimi pale ambapo naongoza kama mkuu wa Wilaya sihitaji
kuondoka na laana za wananchi kwamba nilishiriki kwenye tathimini na wananchi
wakaibiwa hela zao kwa sababu haya ambayo yamefanyika siyo mfano mzuri”.

“Mhe.
Rais ataka haki hii michezo ifike mwisho na mimi nitawaandikia barua maalum
TANROADS, mthamini mkuu wa serikali pamoja na Manispaa hii, hili haliwezekani
wananchi wanathaminishiwa haki yao inakuwa A halafu anakuja kulipwa B kwahiyo
Manispaa nawaagiza kuja kuweka kambi hapa mrudi hapa mpige kambi na nawapatia
Mwezi huu wa nne narudia tena mrudi hapa mpige kambi kwahiyo nikirudi hapa
kwenye mkutano wangu mwananchi akisimama kuzungumzia tathimini kuwa na majibu”.
amesema DC Mtatiro

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili
Julius Mtatiro pia amesema haridhishwi na utendaji wa wakala wa barabara za
vijijini na mijini TARURA Wilaya ya Shinyanga katika utekelezaji wa miradi yao.

“Kati
ya eneo ambalo siridhishi toka nimekuja hapa kama mkuu wa Wilaya, siridhishi na
utendaji wa TARURA kuna maeneo mengi nakwenda kuna miradi mingi nimekwenda
ambayo wakandarasi wanapaswa kuwa site lakini hawako site na siyo tarafa hii
peke yake tarafa zote nilizopita nadhani kuna shida kwahiyo mimi nasema hii
kasi ya utendaji wa TARURA Shinyanga siridhishwi nayo na wakiendeleea namna hii
tutamtaarifu mkurugenzi mkuu maana hawa wakandarasi waliopewa  fedha ambazo ni fedha za walipa kodi fedha za
nchi yetu watekeleza matengenezo ya barabara mbalimbali za Shinyanga wanapaswa
kuwa site Shinyanga ni Manispaa hauwezi kuja hapa tu Ibadakuli vijiji havina
barabara kuna shida gani
”.amesema
DC Mtatiro

Aidha DC huyo Wakili Julius Mtatiro
amesikiliza na kupokea kero mbalimbali kutoka wa wakazi wa tarafa ya Ibadakuli  ambapo amewahakikishia wananachi hao kuwa kamati
yake ya kuchunguza na kushughulikia malalamiko itafika katika maene yao kufahamu
zaidi kero zao ili serikali iweze kuchukua hatua haraka.

Pia katika ziara zake DC Mtatiro
ametembelea tarafa mbalimbali sita za Wilaya ya Shinyanga ikiwemo tarafa ya Old
Shinyanga pamoja na tarafa ya mjini ambapo amehitimisha ziara yake katika
tarafa ya Ibadakuli na kwamba ameahidi kuwa kamati aliyoiunda itatekeleza
majukumu yake kwa weledi ili kila mmoja aweze kupa haki yake.

Kupitia mkutano huo
baadhi ya wananchi waliozungumza na Misalaba Media wamempongeza mkuu wa Wilaya
ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwa kutoa nafasi ya kusikiliza kero na
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi,hali wanayoitaja kuwa ni uongozi
uliotukuka.