Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad ametangaza kugombea Urais Visiwani Zanzibar kupitia chama chake cha ACT-Wazalendo.
Amesema, kutokana na imani ya Wazanzibari waliyoionesha katika miaka yote aliyogombea urais wisiwani humo, ameamua kurejea ulingoni kupambana na yeyote atakayepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.