Madaktari bingwa upasuaji magonjwa ya moyo kutoka israel watembelea bonde la ngorongoro

Jopo la Madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo na wauguzi kutoka nchini Israel wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), ikiwa ni sehemu ya mwaliko wa Rais Dk. John Magufuli alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
.

Baadhi ya maofisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakiwa pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji moyo kutoka nchini Israel wanaotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA)

Daktari bingwa wa Upasuaji wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dk. Naizihijwa Majani akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA baada ya jopo la madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na wauguzi 23 kutoka nchini Israel kuwasili uwanjani hapo wakiwa wanaelekea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kutembelea vivutio    

Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya Moyo kutoka nchini Israel Dk. Assa Sagi akizungumzia ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro baada ya kupewa mwaliko huo na Rais Dk. John Magufuli.

 Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Joyce Mgaya akizungumzia ziara ya jopo la madaktari na wauguzi kutoka nchini Israel wanaotembelea vivutio vya utalii pamoja na kujonea utamaduni wa wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo.

Baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya moyo na wauguzi kutoka nchini Israel wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA wakielekea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) kujionea vivutio vya utalii pamoja na utamaduni wa wakazi wa eneo hilo.