Maelfu ya watu wamlilia boniphace makilagi maarufu musoma food, mazishi yafanyika shinyanga viongozi watoa

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mazishi ya mfanyabiashara wa nafaka Bwana Boniphace
Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food yamefanyika leo Alhamis April 6,2023
Nyumbani kwake kata ya Kambarage mjini Shinyanga.

Bwana Boniphace Makilagi aliyefariki Dunia wiki
hii siku ya Jumatatu April 3, 2023 akiwa Jijini Mwanza.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi wa
serikali, viongozi wa Dini, vyama na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga na
nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Mazishi ya marehemu Bwana Boniphace Said
Makilagi yamefanyika  nyumbani kwake ambapo
misa ya mazishi imeongozwa na Padre Benedick Magaba wa kanisa katoliki parokia
ya mtakatifu Gasper jimbo kuu la Dar Es Salaam

Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Bi. Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba huo
amesema serikali itaendelea kushirikiana na familia ya marehemu Boniphace
Makilagi huku akiwasihi
kuendelea kuyaishi meya
aliyoyaacha katika maisha yao ya kila siku.

Aidha baadhi ya viongozi wa serikali na
chama kutoka sehemu mbalimbali akiwemo Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi.
Johari Samizi wameeleza namna walivyoguswa na msiba wa Boniphace Makilagi jina
maarufu Musoma Food huku wakitoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote
walioguswa na msiba huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia tarehe
27.5.2021 Bwana Boniphace Said Makilagi alipata ajali ya gari huko Mpanda Rukwa
akapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na amekuwa
akipata matibabu nchini Kenya na India.

Alipata nafuu  ambapo  kwa nyakati tofauti alikuwa anapata maumivu ya
kichwa, mnamo tarehe 3.4.2023 aliugua ghafla jijini Mwanza na kufariki dunia.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Musoma Food, Boniphace
Said Kate Makilagi alizaliwa 01.06.1967 alifariki dunia 03.04.2023, ameacha
mjane na watoto wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara
Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara
Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony
Mtaka akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said
Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.
Johari Samizi akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara
Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga
Mhe. Esther Makune akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa mfanyabiashara
Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga. 

Viongozi wa
serikali, Dini na viongozi  mbalimbali 
wa
vyama vya kisiasa wakiwa  kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate
Makilagi maarufu Musoma Food
uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini
Shinyanga

Viongozi wa
serikali, Dini na viongozi  mbalimbali 
wa
vyama vya kisiasa wakiwa  kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate
Makilagi maarufu Musoma Food
uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini
Shinyanga

Viongozi wa serikali, Dini na viongozi  mbalimbali wa vyama vya kisiasa wakiwa  kwenye msiba wa mfanyabiashara Boniphace Said Kate Makilagi maarufu Musoma Food uliofanyika leo kata ya Kambarage Mjini Shinyanga