Mahafari ya 14 shule ya sekondari idahina ushetu, waiomba serikali na wadau kushughulikia changamoto zilizopo


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jumla ya wanafunzi 109 kati yao wavulana
57, wasichana 52 wamehitimu kidato cha nne mwaka huu 2023 katika shule ya
sekondari Idahina iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga.

Shule hiyo imefanya mahafari ya 14 ya
wanafunzi  kuhitimu kidato cha nne tangu
kuanzishwa kwake Mwaka 2007.

Mahafari hayo yamehudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM kata ya
Idahina akiwemo Diwani wa kata hiyo Mhe. Mathias Makashi.

Katika risala ya wahitimu iliyosomwa na
Elen Reuben Petro imebainisha mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio na changamoto
huku wakiiomba serikali, wadau, jamii kwa kushirikiana na wazazi kuendelea
kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa
umeme hali inayotanjwa kuathiri afya ya macho kwa wanafunzi, changamoto ya
bomba la maji katika Bweni la wasichana pamoja na changamoto ya ukosefu wa
walimu wa kike.

“Suala
la umeme linaathiri Afya ya macho hasa wakati wa usiku ambapo wanafunzi wengi
tunahangaika kwa kutumia mwanga hafifu wa umeme 
wa jua wengi tunapata changamoto ya macho hasa nyakati za masika”.

“Shule
ya  sekondari Idahina inakabiliwa na
changamoto ya bomba la maji kwenye Bweni la wasichana ambapo linahitajika
kukamilishwa maana wananchi maana wananchi na wazazi wetu tuliwashuhudia
wakisomba mawe, mchanga, kokoto na kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hostel
kwa wasichana tunaomba utusaidie kukamilisha Bweni hilo ili kuondoa changamoto
ya kubanana kwa wasichana katika Bweni moja”.amesema Elen

“Changamoto
ya kukosa walimu wa kike ambao ni msaada mkubwa wa kusikiliza, kushauri na
kutatua changamoto za watoto wa kike hapa shuleni tunaomba utusaidie kupata
walimu wa kike hata wawili”.

“Lakini
pia kwa miaka minne yapo mafanikio katika shule hii ulifanyika ujenzi wa vyoo
vya kisasa, ujenzi wa nyumba 14 vya kisasa, ununuzi wa mashine ya kuchapisha
mitihani, ununuzi wa mashine ya kusaga unga pamoja na uchangiaji mzuri wa
chakula shuleni”.amesema Elen

Akizungumza mgeni rasmi Bwana Julius lugobi
kwa niamba ya mbunge wa jimbo la Ushetu ataendelea kushirikiana katika kutatua
changamoto zinazoikabili  shule ya
sekondari Idahina ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri na
salama.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Idahina
Mhe. Mathias Makashi amewapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu kidato cha nne
huku akiwasihi kutokata tamaa ili waweze kufikia ndoto zao  ambapo pia amewaomba wazazi kutimiza
wajibu  kwa watoto wao na kuhakikisha
wanasoma ili kuwa na Taifa la vijana wasomi.

 

Wahitimu wa kidato cha nne Mwaka huu 2023
katika shule ya sekondari Idahina wakiingia ukumbini.