Mahakama kuamua dhamana ya mwanahabari sebastian atilio kesho, kesi ya marato yaahirishwa hadi oktoba 22


Na Francis Godwin, Iringa

Mwandishi
wa habari Sebastian Atilio anayekabiliwa kwa makosa mawili yaani kutoa
taarifa ya uongo na kufanya kazi ya uandishi bila kuthibitishwa na bodi.

Jana
ilikua ni siku ya kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa na wakili wa THDC
Emmanuel Chengula anaemtetea mwandishi huyo, mapingamizi hayo ni dhidi
ya maombi yaliyopelekwa na jamhuri kumzuia mwandishi huyo kutopewa
dhamana kwa hofu ya usalama wake dhidi ya RAIA wa kijiji cha ifupira.

Pamoja
na hayo mahakama ya wilaya ya Mufindi mbele ya Hakimu Mkazi Edward
Uforo ilisikiliza mapingamizi yote manne na kuahirisha kesi hiyo mpaka
tarehe 25/09/2019 ambapo itatoa maamuzi juu ya hatima ya dhamana ya
mwandishi Huyo wa habari.

Hata
hivyo kesi yake ya msingi itatajwa tarehe 25/09/2019 Mara baada ya
kusomwa kwa uamuzi unaotokana na mapingamizi yaliyo wekwa.

Mwandishi Sebastian Atilio akiingia ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Mufindi


Wakati huo huo kesi
inayomkabili Mwandishi wa habari George Marato imepangwa kusikilizwa
tena  Oktoba 22 na 23 kwa upande wa mashitaka kutakiwa  kuleta ushahidi
wao.


Katika shauri hilo
wakili wa mshitakiwa Thomas Makongo aliwasilisha hoja kwa kutaka
Mahakama itoe amri kwa TAKUKURU  kufuta taarifa yao kwa Umma
waliosambaza wakiandika maneno yenye kuingilia uhuru wa mahakama na
kumuhukumu mteja wake tofauti kilichopo mahakamani.

Hakimu
Ndira wa mahakama ya Musoma amemtaka wakili awasilishe hoja hiyo kwa
kutaja kifungu cha sheria ili Mahakama iweze kuchukua hatua.

wakili ameiomba mahakama kuwasilisha hoja hiyo na kifungu cha sheria Oktoba  22 wakati kesi hiyo itakaposikilizwa tena.