Maisha ya kuwa na jinsia mbili changamoto kwa mary waithera ama james karanja

Maisha ya kuwa na jinsia mbili yamekuwa changamoto kwa Mary Waithera ama James Karanja

Nabii Darlan Rukih wa Kenya ni mmoja wa Wakenya ambao wanatambulika kama watu wenye jinsia mbili ya kike na ya kiume ambaye amejikubali


Kulikuwa na hali ya sintofahamu wakati Mary Waithera ama James Karanja alipozaliwa mwaka 1991, wakunga walinyamaza wasijue cha kumwambia mama yake.

Alizaliwa na jinsia mbili…jinsia ya kiume na ya kike kwa pamoja. Mama yake akitaka kupata kujua mbona mwanae akazaliwa katika hali hiyo?. Shughuli zote za kutanzua hali hii zilimfanya Mary kulazwa hospitalini kwa wiki tatu alipozaliwa. Huo ukawa ndio mwanzo wa safari ya Mary Waithera ama James Karanja kujitambua

Wazazi wa Mary Waithera waliamua kuanza kumlea kama msichana.
Nilizaliwa tatizo

”Kutoka Mwanzo ,nilizaliwa kuwa tatizo,angalaua kulingana na wale waliokuwa karibu nami. Hakuna aliyejua nilikuwa nini”, anasema James Karanja

Baada ya wazazi wangu kutambua kuwa nilikuwa na matatizo hayo,Babangu aliamua,waliamua kunilea akama msichana ili iwapo siku za usoni nitabadilika na kuwa manaumme,basi itakuwa rahisi kufanya hivo.

Hata hivyo hali yangu ilifanya ndoa ya wazazi kuvunjika.

Bababu alituacha akisema kuwa familia yao haijawahi kuzaa mtu wa aina hii na kukataa hata niridhi jina la ukoo wao kwani waliona kama laana.

Ikaishia nimeitwa jina la nyanyangu;mama ya mamangu aliyenilea.Mamangu kutokana na kuvunjika kwa ndoa yake akashikwa na msongo wa mawazo. Hata hivyo maisha ya yeye kunilea yalikuwa magumu, ”Kila nilipokwenda kuchota maji mtoni,nilikuwa nabeba mtungi na bega langu,tofauti na wasichana wengine waliokuwa wakitumia migongo yao.”

”Alinilea kukua kama mwanamke.Alikuwa akinitayarisha kuwa mke mwema.”

Karanja anakumbuka akiwa ‘msichana’ pekee aliyekuwa akiendesha baisikeli katika kijiji chao.

Shule walitaka kuona taulo za hedhi. Alipojiunga na shule ya Upili ya Kikambala,kulifanyika jambo lisilo la kawaida.

”Walitaka kuona taulo zangu za hedhi”…anakumbuka.

Mwalimu alisema singekubaliwa shuleni bila ya taulo hizo.

Nyanya yangu aliamini kuwa ”ndio msichana aanze kupata hedhi,lazima awe amekeketwa.”Hali ya kuwa na jinsia mbili ya kiume na ya kike ya Mary Waithera ama James Karanja (pichani) ilifanya ndoa ya wazazi wake ivunjike

Mwishowe nilijiunga na shule hiyo ila ugumu ukaendelea.

”Walimu walikuwa wakiniita mvulana”.

Ailipofika kidato cha tatu, aliona mwili wake ukibadilika nalipoanza kubalehe. Mabega yakapanuka na sauti ikabadilika. Akawa anaoga usiku wa manane kabla ya wanafunzi wengine ili wasimwone.

Na wasichana wakaanza kupendezwa naye licha ya kuwa alikuwa kiranja wa shule. Baada ya kumwandikia barua kadhaa. Walimu walipozipata barua hizo, akafukuzwa shule kwa madai ya kueneza mapenzi ya jinsia moja.

”Huo ulikuwa mwanzo wa kujitambua kwangu,” Karanja anasema.

Alielekea hospitalini kwa madakatari na kuchunguzwa ili kujitambua.

Baada ya muda,Karanja alikubaliwa kufanya mtihani wake wa kitaifa,akapita na kujiunga na chuo kikuu.

Alifurahi kuwa alikuwa ameondokea vikwazo ila alikosea.

Ugumu wa kujitambulisha

Katika chuo kikuu cha Nairobi, alizuiliwa mara kadhaa na walinzi ili kueleza ikawaje anaitwa jina la kike Mary Waithera ingawa ana muonekano wa mwanaume.

Hata wahadhiri walipokuwa walitaka kujua mbona akaitwa jina la kike na hata kitambulisho chake kina jinsia ya kike wakati alipokuwa akifanya mitihani tofauto.Mara kwa mara akifukuzwa ama kucheleweshwa kufanya mitihani hiyo.

Kutokana na ugumu huo,Karanja alijaribu kujiua mara tatu. Anasema kuwa unyanyapaa ndio ulikuwa kiini cha hayo yote.
Unaweza pia kutazama:


Masaibu ya kuzaliwa na jinsia mbili Kenya

Hata hivyo Karanja anataka kutambulishwa kama mtu wa jinsia mbili.

Kenya kuwasajilia watu wa jinsia moja.

Inakadiriwa kuwa kuna karibu watu 700,000 wa jinsia mbili wanaoishi nchini Kenya.

Ila idadi hii haijarekodiwa na serikali.

”Watu wa jinsia moja hawaonekani nchini. Kwa namna yoyote ile, hawatambuliki kisheria” anasema mbunge Milly Odhiambo.

Milly anasema kuwa ukosefu wa kutambuliwa kisheria unamaanisha kuwa watu wa namana hii hawana haki ya chochote.

Hata hivyo uamuzi wa serikali kuwasajili watu hawa na kuwatambua ipasavyo unaamanisha kuwa watu kama Karanja watapitia changamoto alizopitia.

Shirika la kitaifa la kuwasajilia watu hapo mbeleni liliwasajili watu kama wanaume ama wanawake tu.

Watoto wanaozaliwa na jisnia mbili hudhaniwa kuwa laana kwa familia na huwauwa mara tu wanapozaliwa katika jamii nyinyi barani afrika.

Kenya itakuwa ataifa la kwanza barani Afrika kuwatambua watu hawa amabao wanajiona watu wa kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *