Makamu wa rais kufungua mkutano wa mwaka wa shirika la mashauriano ya kisheria kwa nchi za asia na afrika (aalco)

Eric Msuya – MAELEZO

Makamu
wa Rais mama Samia Suluhu Hassan anatalajia kumuwakilisha Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa 58 wa mwaka wa
Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO)
utakoanza  Jumatatu tarehe 21 hadi 25 Oktoba jijini Dar es Salaam. 


Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga, amesema Mkutano huo utaudhuriwa na Viongozi
mbalimbali wa Serikali kutoka Nchi 48 za Wanachama wa Shirika hilo
pamoja na Masharika mbalimbali ya Kitaifa. 


“Mkutano
huu utakaoanza Jumatatu unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri, Wanasheria
Wakuu wa Serikali toka Nchi Wanachama, Wawakilishi wa Mashirika
mbalimbali ya Kimataifa, Mabalozi wanaowakilisha Nchi zao hapa Nchini na
Viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka Nchi Wanachama” Amesema Mhe.
Mahiga 


Mkutano
huo utaofanyika kwa siku tano, utajadili masuala mbalimbali ya kisheria
za Kimataifa ikiwa pamoja na Changamoto za kisheria zinazoyakabili
Mataifa Wanachama na Kuangalia namna bora ya kushughulikia changamoto
hizo ili kuwa na Dunia yenye Amani, Usalama na Utulivu kwa ajili ya
Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. 


Sambamba
na hilo maswala mengi yatako jadiliwa katika mkutano huo ni, Sheria ya
Kimataifa ya Bahari, Mitandao na Biashara na Uwekezaji, Kuvunjwa kwa
Sheria ya Kimataifa Nchini Palestina, Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya
Amani, Matumizi ya Sheria za Nchi nje ya Nchi na Tume ya Sheria ya
Kimataifa. 


Tanzania
ilijiunga na The Asian – African Legal Consultative Organisation
(AALCO) mwaka 1973 chini ya Uongozi wa Rais Hayati Baba wa Taifa  Mwl.
Julius Kambarage Nyerere, huku Tanzania ikiwa ni mara yake ya tatu kuwa
wenyeji wa kushiriki katika mkutano huu wa Shirika la Mashauriano ya
kisheria kwa nchi za Asia na Afrika 


“Kwa
mara nyingine tena, Tanzania tunakuwa wenyeji kwa mara ya tatu katika
mkutano huu … Nchi yetu ina miaka 46 toka tujiunge na chama hichi,
mafaniko ni mengi na maslahi ni makubwa na mapana tunayoendelea kuyapata
katika chama hiki” Amesema Mhe. Mahiga 


Shirika
la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika ( The
Asian-African Legal Consultative Organisation – AALCO kilianzishwa 
mwaka 1956 ikiwa ni matokeo ya Mkutano wa Kihistoria wa Bangung,
Indonesia tarehe 18-24 April 1995 (Bandung Conference).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *