Makamu wa rais, samia suluhu afungua mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira sadc

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa
Mawaziri wa Kazi na Ajira, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika (SADC), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax,
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Vijana Wanawake na Watoto kutoka Zanzibar,
Maudline Cyrus Castico wakiteta jambo baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri
wa Kazi na Ajira, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa
ameshika tuzo tayari kwa kuwakabidhi baadhi ya Taasisi ambazo zimekuwa zikitoa
nafasi kwa wahitimu kupata mafunzo ya uzoefu kazini, ambayo leo imezinduliwa
katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira, Nchi Wanachama wa Jumuiya
ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Tanzania Breweries Limited (TBL) kwa kuwa Taasisi inayochukua wahitimu wengi
kwenye programu ya mafunzo ya uzoefu kazini(Ineternship) mara baada ya kuzindua
rasmi Programu hiyo ambayo inatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la
kukuza ujuzi wa vijana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwakabidhi vyeti wahitimu wa mafunzo ya uzoefu
kazini waliokuwa wakijitolea katika Taasisi mbalimbali mara baada ya kuzindua
programu hiyo ambayo inatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kukuza
ujuzi wa vijana.

ujuzi wa vijana
Mnufaika wa Programu ya mafunzo ya uzoefu
kazini(Intership) akielezea namna programu hiyo ilivyomsaidia kupata uzoefu wa
kazi, Programu hiyo ambayo inatekelezwa na Serikali ya Tanzania imezinduliwa
rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan, katika Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira, Nchi Wanachama wa Jumuiya
ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania

Katibu
Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt.
Stergomena Tax akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira, Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere(JNICC), Jijini Dar es
Salaam, Tanzania.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista
Mhagama, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, kuzungumza na hadhara ya washiriki wa Mkutano wa Mawaziri
wa Kazi na Ajira, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika
(SADC), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam, Tanzania.