Mama salma kikwete aweka jiwe la msingi jengo la umoja wa vikundi vya wama majohe

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb) leo Jumamosi ameweka Jiwe
la Msingi Jengo la Taasisi ya Umoja Wa Vikundi Majohe(UVIMA) lililopo
katika kata ya Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Said Kumbilamoto kwa naiba ya Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Mwenyekiti wa UWT (W) Ilala Bi Amina Omary George. 
Mhe. Mama Salma Kikwete ameahidi kuchangia Bati 100 ili kusaidia kukamilika kwa ujenzi wa Jengo hilo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) Mhe. Mama Salma Kikwete (Mb) akizungumza wakati wa
akiweka jiwe la msingi jengo la Taasisi ya Umoja wa Vikundi Majohe
(UVIMA) lililopo katika kata ya Majohe Manispaa ya Ilala jijini Dar es
salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *