Mamia wajitokeza kuomba ridhaa ya ubunge ndani ya ccm

Picha ni
Kabula Juma Sukwa akiwa kwenye ofisi za UWT mkoa akiwa na Katibu wa
mkoa wa umoja huo akipokea fomu za kugombea nafasi ya ubunge wa viti
maalum kupitia umoja huo leo jijini Arusha.

Pichani
ni Kabula alipowasili kuchukuwa fomu akipata maelekezo na.utaratibu
kabla ya kukabidhiwa fomu leo jijini Arusha.

Pichani
ni Mfanyabiashara Maarufu Mustafa Panju akipokea fomu ya kugombea
nafasi ya ubunge mapema leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud
Arusha

Pichani ni wakili Maarufu Albert Msando akipokea Fomu kutoka kwa
katibu wa CCM wilaya ya Arusha Denis Mwita leo jijini Arusha picha
zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Wakati wagombea wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha mapinduzi
wakichukuwa fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kupeperusha bendera
ikiwa siku ya pili Leo huku wagombea wakifika 69 ndani siku
mbili.
Mvuto huo umekolezwa leo baada ya wakili maarufu Albert Msando
kuchukuwa fomu kuomba ridhaa ya wanachama kugombea nafasi hiyo kupitia
chama hicho ikiwa ni mlolongo wa wagombea akiwemo Philemon Mollel
Mrisho Gambo na Kalist Lazaro waliochukuwa jana.
Aidha katika nafasi ya viti maalum kupitia umoja wa wanawake UWT yupo
mwanadada maarufu Kabula Juma Sukwa ambaye ameonyesha njia kwa
wanawake wengine kuomba ridhaa hadi jioni ya leo zaidi ya kinamama 39
wamejitokeza kuomba nafasi hizo.
Duru za kisiasa mkoani hapa zinaonyesha kuwepo kwa kimuhemuhe na
wanachama wanakazi kubwa kuona nani ni nani kujua atapitishwa na chama
hicho kuopeperusha bendera kwenye bunge lijalo.
Hata hivyo mchuano utakuwa mkali kwa wagombea kutokana na wingi wao
kila moja akionyesha nia ya kutaka kuhudumia wananchi kupitia nafasi
za ubunge ndani ya chama hicho kikongwe nchini.