Mamia wajitokeza uzinduzi msimu wa kilimo njombe

Na Joctan Agustino, Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Luth Msafiri amezindua rasmi
msimu mpya wa kilimo 2019/2020 katika Halmashauri ya Mji wa Njombe
akiwataka wakulima kuhakikisha Wanapima udongo ili kuongeza mavuno
zaidi.

Uzinduzi huo
Umefanyika katika Kijiji na kata ya Uwemba ambapo
uliambatana na maonyesho ya Pembejeo za kilimo kutoka kwa wadau wa sekta
ya kilimo mjini humo.

Pamoja
na mambo mengine Mh Luth Msafiri amewaonya mawakala wa Pembejeo za
kilimo wenye tabia ya kuwauzia wakulima Pembejeo feki  na wale
wanaopandisha bei kiholela.

Bi
Luth Msafiri Alisema kuwa Hatowavumilia wafanyabiashara wote wa
Pembejeo za kilimo wanaojihusisha na vitendo vya dhuluma kwa wakulima
kwa kuwauzia Pembejeo Feki hususani Mbegu za Mazao Mbalimbali.

Maonyesho
hayo yalibeba kauli mbiu inayohamasisha wakulima wote kuwa na utaratibu
wa kupima udongo kabla kupanda mazao yao Shambani kwa lengo la kuongeza
Uzalishaji.

Uzinduzi kama huo umefanyika katika Halmashauri zote za Wilaya ya Njombe.