Matumizi ya mfumo wa kuweka kumbukumbu utasaidia kupunguza malalamiko ya wanufaika wa tasaf

 


OFISA anayshughulikia malalamiko wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Makwinja Dismas Yusuph akizungumza wakati wa mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga

Watendaji wa TASAF kutoka Halamshauri 35 waliohudhuria mafunzo hayo ya siku mbili wakifuatilia matukio mbalimbali

Na Mashaka Mhando,  Tanga
 
MATUMIZI
ya mfumo wa kuweka kumbukumbu, utasaidia kupunguza malalamiko ya
wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia mradi
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumza
katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa TASAF kutoka
halmashauri 35 za mikoa ya Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha na
Pemba, Ofisa anayeshughulikia malalamiko wa mfuko huo, Makwinja Dismas
Yusuph alisema mfumo huo utapunguza malalamiko kwa kiasi kikubwa. 
“Madhumuni
ya mafunzo haya kwa watendaji wetu kutoka halmashauri za wilaya na
majiji 35, utasaidia kupunguza malalamiko ambayo mara nyingi yamekuwa
yakitolewa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini,” alisema
Makwinja. 
Alisema mpango
wa kunusuru kaya masikini wamekuwa wakitoa ruzuku kwa kaya
zinazostahili kwa kukidhi vigezo vya elimu, afya na lishe. 
“Sasa
unapokuwa na mradi kama huu (Social Protection)  lazima unazalisha
malalamiko mengi kwasababu unagusa jamii moja kwa moja na malalamiko ni
mengi, ” alisema. 
Ofisa
huyo alisema kufuatia hali hiyo mpango umeweka kitengo maalum (Call
Center) chenye wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali
utakaoshughulikia malalamiko yatakayotolewa. 
Alisema
kitengo hicho kitapokea simu za malalamiko, itayachunguza kama yana
ukweli kisha watayapatia ufumbuzi tofauti na utaratibu wa zamani wa
kupokea taarifa zilizoandikwa kwenye makaratasi. 
Makwinja
alibainisha miongoni mwa malalamiko yanayotolewa mara kwa mara na
wanufaika hao, ni pamoja na kukatwa fedha zilizotokana na wao kushindwa
kukidhi vigezo vilivyowekwa na mfuko. 
“Hapa
ni lazina niseme kwamba sababu kubwa ni elimu kwa wanufaika maana
wakati mwingine wanakiuka taratibu tulizoziweka hasa katika suala la
elimu, afya na lishe, ” alisema Makwinja na kuongeza, 
“TASAF
haigawi fedha tu kama wengi wanavyodhani, tunahaulisha kwa kutoa ruzuku
kiasi kidogo cha fedha ili kuleta matokeo katika kaya masikini kwa
kiwango kidogo wanachopewa, ” 
Alisema
fedha hizo wanataka zilete tija kwa wanafamilia kwa watoto kwenda
shuleni na kuhudhuria masomo kwa kiwango cha walau asilimia 80, kupata
huduma za afya pamoja na lishe bora. 
Hata
hivyo, ofisa huyo aliwataka watendaji waliopatiwa mafunzo hayo waone
wajibu wa kile walichojifunza wakakitekeleze kwa kutumia ujuzi
utakaosaidia mradi huo kuwa na kumbukumbu sahihi zitakazohifadhiwa kwa
njia ya eletroniki. 
Hadi sasa mfuko wa Tasaf umeweza kuhudumia Kaya masikini zipatazo milioni moja na laki moja nchini kupitia mpango huo (SDGs). 
 
MWISHO