Matumizi ya vifaa vya kisasa vilivyowekezwa na osha vitasaidia kupunguza malalamiko sehemu za kazi-mhe.massawe

 

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu,
ndugu Andrew Massawe akizungumza kwenye mafunzo kwa wakaaguzi wa OSHA
yaliyofanyika jijini DodomaKatibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Andrew
Massawe akifanya kipimo cha macho kwa kutumia kifaa kipya cha VT 1
Master Badhii
ya Wakaguzi wa OSHA wakifuatilia kwa makini mafunzo maalamu ya kipimo
cha macho ya namna ya matumizi ya kifaa cha VT1-Master Baadhi ya Wakaguzi wakifuatilia kwa Viendo mafunzo jinsi ya kutumia kifaa cha VT1 Master.

************************************* 

Mwandishi wetu,DODOMA

 Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, ndugu
Andrew Massawe, amesema matumizi ya vifaa vya kisasa ambavyo OSHA
imewekeza, itasaidia sana kupunguza malalamiko sehemu za kazi, kutokana
na kuwa na majibu yenye uhakika Zaidi.

 Akizungumza kwenye
ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na OSHA maalamu kwa
wakaguzi wa Afya toka OSHA, yaliyofanyika jijini Dodoma, Massawe amesema
matumizi ya vifaa vipya vya kisasa hususani kipimo hiki cha macho
ambavyo taasisi hiyo imewekeza itasaidia sana kupunguza malalamiko ya
baadhi ya wafanyakazi, kutokubaliana na majibu ya vipimo ambavyo
wanapatiwa, na vile vile itasaidia kuwafikia watu wengi. 

 “kitendo
cha taasisi hiyo kuwekeza kwenye vifaa vya kisasasa ni jambo la
kupongezwa na ni jambo zuri, amesema taasisi hivyo kuwa na vifaa hivyo
vya kisasa ambavyo ni maalumu kwaajili ya kupima uwezo wa macho kuona,
aidha Katibu Mkuu huyo amewataka OSHA kuangalia namna pia ya kupata
vifaa vya vingine vya kisasa kwenye maeneo mengine”alifafanua ndugu
Andrew Massawe. 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija
Mwenda amesema lengo la mafunzo hayo ni sehemu ya program ya taasisi
hiyo kuwajengea uwezo Zaidi wakaguzi wa Afya wa OSHA, na mafunzo ya leo
yalikuwa maalumu juu ya matumizi ya vifaa vipya vya kupima macho ambavyo
taasisi hiyo imenununua. 

Bi.Mwenda amesema vifaa hivyo vya macho
ambavyo kitaalamu vinajulikana kama VT 1 master ambacho taasisi hiyo
imenunua ni vya kisasa Zaidi, na vina wigo mpana Zaidi wa kutoa majibu
tofauti na kifaa cha snell chart ambacho chenyewe kina uwezo wa kupima
uwezo wa macho kuona mbali au karibu tu, hivyo kushindwa kubainisha
changamoto zingine za macho zinazomkabili mtu, kama vile kushindwa
kutofautisha rangi, kuona usiku.

 “ Kazi yetu pia ni kufanya
uchunguzi wa ajali sehemu za kazi zinapotokea,tathimini ndogo
tulioifanya, tuliona kuwa ajali nyingi zinazotokea sehemu za kazi,
ukiwauliza wahusika wanakuambia hakuona kilichotokea, tukaona kwamba
kumbe mtu anaweza akawa na matatizo ya macho bila yeye kujua na hivyo
kusababisha ajali , ”

 Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dr Robert
Mazengo amesema vifaa hivyo vya kupima macho ambavyo OSHA, imevipata ni
vifaa vya kisasa zaidi, na vinauwezo mkubwa zaidi wa kubaina mambo
mbalimbali ambayo yatasaidia kuwashauri waajiri zaidi. 

Kwa upande
wao washiriki wa mafunzo kutoka OSHA Bi Amina Nangu na Daktari Rajabu
Mambo, wamesema, wao kama wakaguzi matumizi ya vifaa hivyo kwa vitakuwa
msaada sana, kwani vitasaidia kutoa majibu yenye uhakika Zaidi na
vitaokoa muda kwani, kifaa hicho kinauwezo wa kupima watu wengi Zaidi
kwa wakati mmoja, tofauti na kifaa cha zamani ambacho ni Snells Chart.