Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, Freeman Mbowe anaumwa na amelazwa
katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam tangu Novemba 17,
2019.

Mbowe ni miongoni mwa viongozi tisa wa Chadema wanaokabiliwa na kesi ya
uchochezi namba 112/ 2018 inayoendelea leo Jumanne Novemba 19, 2019 kwa
hatua ya utetezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Alitakiwa kuendelea kujitetea leo lakini mdhamini wake, Greyson
Selestine ameieleza mahakama hiyo kuwa mbunge huyo wa Hai anaumwa na
amelazwa katika hospitali hiyo.

“Mbowe amelazwa tangu Novemba 17 katika hospitali ya Aga Khan,” amesema
Selestine bila kueleza mwenyekiti huyo wa Chadema anaumwa nini.

Kinachoendelea katika kesi hiyo ni washtakiwa wanne, mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche; Ester Bulaya (Bunda), Mchungaji Peter Msigwa
(Iringa Mjini) na Halima Mdee (Kawe) kujitetea kwanini wasifutiwe
dhamana.

Ijumaa iliyopita Novemba 15, 2019, mahakama hiyo ilitoa amri ya
kukamatwa kwa washtakiwa hao kutokana na kukiuka masharti ya dhamana
baada ya kutofika mahakama kusikiliza kesi hiyo.