Mbunge kibaha vijijini atoa hekari kumi ujenzi wa shule ya sekondari…

Mbunge wa Jimbo la Kibaha
Vijijini Hamoud Jumaa kushoto akikabidhiwa zawadi ya fimbo  na mmoja wa
viongozi wa jamii ya wafugaji alipowasili katika kijiji cha Kigoda,
kulia kwake ni Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia William Ole
Nasha baada ya kuwasili katika eneo hilo  kwa lengo la kuweka jiwe la
msingi katika ofisi ya kijiji hicho pamoja na kutembelea eneo ambalo
limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Naibu waziri wa elimu sayansi na
teknolojia wa kati kati akipiga makofi katika halfa ya uwekaji wa jiwe
la msingi katika ofisi ya kijiji  cha kigoda kilichopo kata ya Gwata
katika halmashauri ya Kibaha vijini kushoto kwake ni Mbunge wa Kibaha
Vijijini Haoumd Jumaa, na viongozi wengine wa kijiji hicho.(PICHA NA
CICTOR MASANGU)
Naibu waziri wa elimu William Ole
Nasha kushoto akiwa katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi pamoja na
kutembelea eneo la ambalo limetengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa
shule mpya ya kata ya Gwata.kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha
vijijini Haoumd Jumaa.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Mbungewa Jimbo la Kibaha vijijini
Haoumd Jumaa akizungumza na baadhi ya wananchi wa  kata ya Gwata hawapo
pichani wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa
ujenzi kwa ajaili ya ofisi ya kijiji cha kigoga pamoja na kujoinenea
eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata(PICHA NA
VICTOR MASANGU).
***********************************NA VICTOR  MASANGU, PWANI  
Naibu Waziri wa elimu sayansi
na teknolojia  Williamu Ole Nasha amechukizwa kuona vitendo vya baaadhi
ya wazazi wa jamii ya wafugaji kutothamini suala la elimu na kuamua
kuwaozesha watoto wao mapema na kuwatumikisha katika kazi za kuchunga
mifugo ambapo amekemea  na kulaani vikali vitendo hivyo na kuwataka
kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule ili  kuunga mkono juhudi za
serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu ikiwemo utoaji wa elimu
bure..
Ole Nasha ametoa kauli hiyo 
wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa
ofisi ya serikalI ya kijiji cha Kigoda kilichopo katika kata ya Gwata
Wilaya ya Kibaha sambamba na  kutembelea eneo maalumu ambalo 
limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari  ya kata ambayo
itaweza kuwa mkombozi mkubwa  kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea
umbari wa kilometa nane kwenda kutafuta huduma ya elimu  katika maeneo
mengine.
Aliongeza kuwa  lengo la serikali
ya awamu ya tano ni kuboresha sekta ya elimu katika ngazi zote hivyo
kitu kikubwa ni kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi bora ikiwemo
kuwapeleka shule lengo ikiwa ni kuwapatia ujuzi na mahalifa ambao
utaweza kuliletea taifa maendeleo.
“Nampongeza sana Mbunge wa jimnbo
la Kibaha Vijijini kwani amekuwa ni mtu mwenye kunisumbua  sana lakini
lengo lake kubwa ni kuwaletea maenedeleo wananchi wake, kwa hiyo kikubwa
zaidi tumuunge mkono katika kuleta mabadiliko na hili tabia ya
kuwaozesha watoto wenu kwa kweli mimi nataka muiache kabisa na
kuwachungisha ng’ombe,”alisema.
Mmoja wa  wazazi wa jamii ya
wafugaji  akizungumza kwa niaba ya wenzake aliahidi kulitekeleza na
kulivalia njuga agizo ambalo limetolewa na Naibu Waziri na kwamba
wataweka mipango madhubuti ya kuwapatia watoto wao haki zao za msingi
ikiwemo kuwapeleka shule pamoja na kuachana na tabia ya kuwatumiksiha
kwa kipindi kirefu katika kuchunga
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha
vijijini Hamoud Jumaa katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk.
John Pombe ,Magufuli katika sekta ya elimu ameamua kutoa eneo la hekari
kumi  pamoja na kuahidi ujenzi wa madarasa mawili kwa lengo la kuanzisha
mradi wa ujenzi wa shule ya kata ya Gwata ambayo itapunguza kwa  kiasi
kikubwa  adha  na kero kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitumia muda wao
mwingi wakiwa njiani kuelekea shuleni.
“Kwanza kabisa napenda kumpongeza
Naibu waziri wa elimu kwa kuja kufanya ziara katika kijiji hiki na mimi
napenda kumuahidi kuwa maelekezo yake yote ya kuongeza hekari zingine
mimi nipo tayari kwa hiyo mimi ninatongeza hekari zingine tano kwa hiyo
jumla zitakuwa kumi hii yote ni kuhakikisha tunaunga mkono juhudin za
serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu,”alisema Jumaa.
Aidha Jumaa katika hatua nyingine
amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba analeta mabadiliko chanya
ya kimaendeleo katika Nyanja mbali mbali na kwamba atashirikiana bega
kwa bega na wananchi pamoja  na serikali kwa jili ya kukamilisha mradi
wa ujenzi wa shule hiyo ya kata ya Gwata ambayo itakuwa ni msaada mkubwa
katika kuwaondolewa wanafunzi changamoto ya kutembea umbari mrefu.
Pia aliwaasa wazazi na walezi wa
jamii ya wafugaji kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dr.John  Pombe
Magufuli katika kuhakikisha kwamba watoto wote wenye umri wa kwenda
shule wanapelekwa mara moja ili kuwapatia haki yao ya msingi pamoja na
kuwataka kuachana na tabia ya kuwakatisha masomo bila sababu zozote za
msingi.
Kumekuwepo na wimbi la baadhi ya
jamii ya wafugaji katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuamua
kuwakatisha watoto wao masomo na kuwatumikisha katika kazi mbali mbali
ikiwemo kuwapeleka maporini kwa ajili ya kuchunga ng’ombe na mbuzi
pamoja na wengine kuwaozesha kitu ambacho kinawanyima kupata haki zao za
msingi ikiwemo suala la elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *