Mbunge neema lugangira aibua mjadala mamilioni kutumika kila mwezi kulisha chakula mahabusu

 

 

MBUNGE
wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mhe Neema
Lugangira akizungumza wakati akichangia mchango wake Bungeni Jijini
Dodoma wa kuboresha Mpango wa
Maendeleo ya Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa
ya kuwalisha chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe
kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
 MBUNGE
wa Viti Maalumu CCM kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs); Mhe Neema
Lugangira ameibua mjadala mpya kuhusu mamilioni ya fedha ambazo zimekuwa
zikitumika kila mwezi kulisha chakula mahabusu hapa nchini baada ya
kuishauri Serikali ichukue maamuzi madhubuti ya kuona namna ya kupunguza
idadi ya mahabusu waliopo magerezani ili kupunguza gharama hizo
zinazotumika.

Mbunge Neema ameibua mjadala huo wakati akichangia
mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wa kuboresha Mpango wa Maendeleo ya
Taifa uliojikita kuishauri Serikali kupunguza gharama kubwa ya kuwalisha
chakula mahabusu ili fedha zitakazookolewa zielekezwe kwenye
utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.

Alisema iwapo idadi hiyo
ikipunguzwa itasaidia kuokoa fedha ambazo hivi sasa Jeshi la Magereza
linatumia Milioni 900 kila mwezi  kwa aili ya chakula cha Wafungwa na
Mahabusu zitasaidia katika masuala mengine mbalimbali ya kimaendeleo
hapa nchini.

Mbunge Neema alisema alisema anaamini kwamba
wanapozungumzia kuchangia kuboresha Mpango wa Maendeleo ya Taifa ni
lazima pia waangalia namna ya kupunguza mzigo usiokuwa na lazima kwa
Serikali na ili Fedha zitakazookolewa ziekelezwe eneo jingine ambalo
linastahili kwa sababu yeye binafsi anaona huo ni upotevu wa Fedha
ambazo sio za lazima.

“Pamoja na ushauri huu Mh Naibu Spika
nashauri njia nyengine ambazo Serikali inaweza kufanya ni Mahakama ibebe
jukumu la kugharamia Bajeti ya kulisha mahabusu waliopo gerezani kwa
sababu kimsingi wapo huko kutokana na ucheleweshwaji wa ucheleweshwaji
wa kesi zao kupata
hukumu” Alisema Mbunge Neema

Aidha, Mhe
Neema Lugangira aliongeza kwamba hata Jeshi la Polisi pia pengine
linajukumu kwenye hili kwa sababu bila kufanya hivyo ni kuendelea
kulionea Jeshi la Magereza wakati Serikali imesema lijitegemee wakati
halina vyanzo mapato hivyo ni matumaini yake kwamba wakati Waziri wa
Fedha
na Mipango, Mhe Mwigulu Nchemba atakapo wasilisha muelekeo kulingana na
maoni mengi yaliyotolewa atazingatia ushauri wake maana jambo hili
analijua vizuri sana ukizingita alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
na Waziri wa Katiba na Sheria.

“Kwani ni lazima Serikali ifika
mahali iangalie suala la idadi kubwa ya mahabusu waliopo gerezani na
nasema hivyo kwa sababu hivi sasa Tanzania ina wafungwa takribani 16,836
na mahabusu 16,703 ambapo Jeshi la Magereza kila mwezi inatumia milioni
900 kwa ajili ya kuwalisha wafungwa na mahabusu hiyo ni gharama kubwa
sana kwa serikali” Alisema Mbunge Neema

“Sasa tupate picha kidogo
ikiwa tutaweza kupunguza idadi kubwa ya mahabusu gezerani inamaana kati
ya hiyo milioni 900 kila mwezi inayotumika na Jeshi la Magereza kwa
ajili ya  kulisha chakula wafungwa na mahabusu tukiweza kupunguza
idadi ya hao mahabusu ina maana kuna kiasi kikubwa cha fedha kinaweza
kuokolewa na kiasi hicho iila mwezi kitakwenda kufidia kiasi kikubwa cha
fedha ambacho kinahitajika ili kutekeleza mipango mbalimbali na ushauri
uliotolewa na wabunge” Alisema Mbunge Neema Lugangira.

Mhe
Neema Lugangira alikumbushia pia Hotuba za hivi karibu za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Rais Samia Suluhu Hassan
aliliongelea suala la idadi kubwa ya mahabusu kwenye magereza hivyo ni
matarajio yake jambo hili litapewa uzito unaostahili.