Mbunge neema lugangira aiomba serikali iikaribishe sekta ya asasi za kiraia kama ilivyofanya kwa sekta binafsi

 


MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Mhe. Neema Lugangira akichangia kwenye Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo alijiwekeza kwenye mambo mawili ya Lishe na Sekta ya Asasi za Kiraia (NGOs, CSOs na CBOs)
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM)
kupitia Kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Mhe. Neema Lugangira akichangia  kwenye Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu ambayo alijiwekeza kwenye mambo mawili ya Lishe na Sekta ya Asasi
za Kiraia (NGOs, CSOs na CBOs)


MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM)
kupitia Kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Mhe. Neema Lugangira
ameiomba Serikali iikaribishe Sekta ya Asasi za Kiraia kama
ilivyowakaribisha Sekta Binafsi kutokana na  utayari wao kushirikiana na
Serikali .

Aliyasema
hayo leo wakati akichangia kwenye Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu ambayo alijiwekeza kwenye mambo mawili ya Lishe na Sekta ya Asasi
za Kiraia (NGOs, CSOs na CBOs) ambapo alisema awali alikuwa na hofu juu
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kumezwa na Afya.  
 
Hata
hivyo alisema anamshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kulitambua hili na kuweka naibu waziri anayesimamia Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto hatua ambayo itakuwa chachu ya kufanikisha
Mipango ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

 
Mhe
Neema Lugangira alisema pia Sekta ya Asasi za Kiraia ina mchango mkubwa
kwa sababu inaajiri watu wengi sana na kwa Taarifa ya Wizara ya Afya
2017 katika Mashirika 300 yalichangia zaidi ya  ajira 5517 Sekta ya
Asasi za Kiraia na inadhihirisha kwamba hiyo ni tanuri la kuandaa
Viongozi wa Kitaifa kuanzia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Mhe Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa, 
 

Aliwataja
wengine kuwa ni Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Prof Palamagamba Kabudi;
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe Ummy Mwalimu; Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Uwekezaji Mhe Prof Kitila Mkumbo;  Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Suleiman Jafo; Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Ole Nasha; Naibu Waziri wa Ofisi ya
Waziri Mkuu – Watu wenye Ulemavu Mhe Ummy Nderiananga na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe Prof Adelardu Kilangi

Mbunge
Neema alielezea kwamba Sekta hiyo ina mchango mkubwa hivyo ushirikiano
wao na Serikali utaweza kuleta tija kubwa na kuweza kuwa chachu ya
Maendeleo ya Taifa ambayo ni muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wake na
wananchi

Mbunge
Neema alisema hivi sasa Sekta ya Asasi za Kiraia wanakusudia kuandaa
Mpango Kazi ambao watauwasilisha kwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa
Majaliwa kabla ya kwenda kumuona Mhe Rais kama ambavyo alishaomba.

Kwa
kumalizia, Mhe Neema Lugangira alimaliza kwa kusema ndani ya Bunge wapo
Wabunge wengi waliopitia Sekta ya Asasi za Kiraia hivyo anaona ipo haja
ya kuanzisha Kikundi cha Wabunge wa Vinara wa Azaki yaani NGOs, CSOs na
CBOs ili kuimarisha Utekelezaji wa Muongozo wa Uhusishwaji Asasi za
Kiraia kwenye Kamati za Bunge ambao umeandaliwa na Bunge.

Hata
hivyo alisema kwamba Asasi za Kiraia inapenda kuipongeza Serikali kwa
wito wa utashi wa kushirikiana na Sekta Binafsi ili kukuza Ustawi wa
Maendeleo ya Jamii na Uchumi wa Taifa.
 
“Nitumie
fursa hii kuikimbusha Serikali kwamba kuna Sekta nyengine ambayo nayo
inaweza kuchangia kwenye maeneo ya Taifa ambayo ni Sekta ya Asasi za
Kiraia (NGOs, CSOs) kwa sababu sekta hiyo inasifa zote za kuwa chachu ya
kuinua na kukweza Dira ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa” Alisema


Alisema
hata kwenye Ilani ya CCM imetambua mchango mkubwa wa Asasi za Kiraia
kwamba ni muhimu katika kutekeleza mipango ya maendeleo na alifanya
rejea ukurasa ya 24 na 128 lakini vivyo hivyo alisema kwamba CCM ndio
Chama pekee ambacho kimetenga kwenye nafasi zake za Ubunge Viti Maalumu
kuwa Mwakilishi wa Kundi la Asasi za Kiraia ambapo yeye anawakilisha
Tanzania Bara na Mhe Khadija Abood anawakilisha Zanzibar.

“Lakini
pia napenda kuipongeza Serikali kupitia Msajili wa NGOs kwa kazi kubwa
inayofanya kusimamia Utekelezaji wa Sheria za NGOs 2019 na kwa mara ya
kwanza imeweza kuchakata na kubainisha ni kiasi cha fedha kinachoingia
nchini kwenye sekta hiyo” Alisema

Mbunge
Neema alisema  kwa kipindi cha miezi sita tu kati ya Julai 2020 Machi
2021 Jumla ya mikataba 178 ilichakatwa na ilifanyiwa upembuzi na ofisi
ya Msajili wa NGOS iliweza kubaini jumla ya TZS 546,758,508,322.27 yaani
Bilioni 546 Milioni 758, Laki 508 ziliingia nchini kupitia NGOs hivyo
Sekta hiyo ina mchango mkubwa sana katika kuendeleza Taifa.


Mbunge
Neema aliomba pia itengwe Bajeti ya kutosha kwa Ofisi ya Msajili wa
NGOs na Baraza la Taifa la NGOs ili waweze kuendelea kusimamia
utekelezaji na utaratibu kwenye sekta hiyo muhimu kwa Maendeleo ya Nchi.
 

Mwisho