Mmbunge neema lugangira aitaka serikali kuandaa kanuni za kumlinda mlaji “food labelling


MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akiwa Bungeni Jijini Dodoma leo

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe
Profesa Kitila Mkumbo akijibu hoja mbalimbali

NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs)
Neema Lugangira ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara itoe Kanuni za
Food Labelling zitakazowalinda walaji na sio kuendelea kuweka maisha ya
Watanzania rehani.
Ameyasema
hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya
Viwanda na Biashara kupitia Mchango wa Maandishi na Taarifa aliyotoa
ambapo alisema hilo linatokana na hivi sasa kuwepo kwa changamoto ya
Usalama wa Chakula yaani Food Safety unaochangiwa na baadhi ya majukumu
ya TFDA ya kupelekwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Akichangia
kupitia Mchango wake wa Maandishi Mbunge Neema Lugangira alianza kwa
kuikumbusha Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa moja ya majukumu yake ni
kufuatilia na kutathimini utendaji katika viwanda, biashara, masoko,
viwanda vidogo vidogo na biashara ndogo ndogo ikiwemo taasisi
zinazowezesha maendeleo viwanda na biashara.
Alisema
sanjari na jukumu hilo baada ya Marekebisho ya Sheria ya Viwango ya
Mwaka 2009 iliyochukua majukumu ya TFDA na kuyahamishia TBS ikiwemo
jukumu la kusimamia Ubora na Usalama wa Chakula .
Aidha
alisema Wizara ya Viwanda na Biashara  imefanya kazi kubwa ya
kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda vya kuchakata na kusindika vyakula
nchini na inastahili pongezi kubwa lakini kuna changamoto katika eneo la
Usalama wa Vyakula nchini.
“Nasema
hivi kwa sababu nyanya inaweza kupuliziwa dawa siku kama ya jana na
ikavunwa leo leo au kesho nyanya hiyo ikiuzwa sokoni mwananchi akainunua
na kutengeneza kachumbari na akala jambo ambalo linaweka hatarini
maisha yake kutokana na chemikali hatari zilizopo kwenye nyanya” Alisema
Mbunge
Neema Lugangira aliongeza kuwa wakati mwengine wananunua juisi ya box
kama ya juisi ya chungwa wakiamini juisi ile ni ya chungwa halisi lakini
mara nyingi kinachokuwepo ndani ni Concentrate, rangi, ladha na sio
chungwa halisi pia kiwango cha sukari kinachokuwepo ni hatari sana.
“Huu
ni mfano ambao unaweza kupelekea udanganyifu mkubwa unaochangia kwa
kasi ongezeko la tatizo la uzito uliozidi na viribatumbo nchini hususan
kwa watoto wadogo ambao ni wanywaji wakubwa wa juisi ni za box.
Katika
mfano mwingine Mbunge Lugangura alisema wananchi tunanunua Yoghut ya
Strawberry tukiamini ndani kuna Strawberry halisi jambo ambalo mara
nyingi sio kweli bali kinachokuwepo ni rangi na ladha japo kwenye kopo
la Yoghurt/Mtindi inakuwepo picha ya tunda la Stawberry.” Alisema
Mbunge
alisema hali hiyo ipo hata kwenye bidhaa za vyakula zingine ikiwemo
mafuta ya kupikia, ice cream ambapo changamoto hiyo inawezeshwa kwa
kiasi kubwa na Mfumo wa sasa wa kuweka lable/lebo kwenye Vifungashio vya
Chakula yaani Food Labelling; jambo ambalo linaweza kuhatarisha Maisha
ya Watanzania kwa sababu hivi sasa wengi wetu tunanua bidhaa za vyakula
pasipo kuelewa nini haswa kimo ndani yake hivyo hatujui usalama wake.
Aliongeza
kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara inalo jukumu la moja kwa moja la
kuimarisha Usalama wa Vyakula vinavyochakatwa na kusindikwa na viwanda
na biashara zilizochini ya Wizara na kutokufanya kitu na kuendelea
kuweka Maisha ya Watanzania Rehani.
“Kwa
mantiki hiyo ningependa kukushauri wewe kama Waziri wa Viwanda na
Biashara uandae Kanuni za Food Labelling zitakazoweka ulazima wa
wachakataji na wasindikaji wa vyakula kuandika wazi kilichopo ndani na
takwa hilo liwe kwa bidhaa za vyakula zinazozalishwa nchini na
zinazotoka nje ya nchi” Alisema Mbunge Lugangira 
Hata
hivyo alisema kama wameweza kufanya hivyo kwa Sigara ambazo juu yake
pakiti inasema wazi uvutaji wa sigara ni hatari kwa maisha yako kwanini
wasindwe kwenye bidhaa za vyakula?
Mbunge
Neema alisisitiza pia umuhimu wa Wizara kuanzisha Kampeni ya Elimu kwa
Umma ya kuwaelimisha jamii maana ya Food Labelling watakazopendekeza
kupitia Kanuni ili kila Mtanzania aweze kufanya maamuzi sahihi kutokana
na manunuzi ya chakula jambo ambalo hata Chama cha Mapinduzi imegusia
kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025 Ibara ya 49(7) ukurasa
wa 61 kwa kusema “CCM itaelekeza Serikali kubuni na kuendeleza mikakati
ya uhamasishaji wa Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozakishwa
katika viwanda vya ndani” na hii lazima iende sanjari na kumlinda mlaji
atakae nunua bidhaa za vyakula. 
Mbunge
Neema Lugangira alimalizia kwa kusema ni matarajio yake Wizara ya
Viwanda na Biashara itafanyia kazi ushauri wake na Tanzania inaweza
kujifunza toke nchi zingine kama Chile.
Wakati
wa kuhitimisha Hoja yake ya Bajeti, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe
Profesa Kitila Mkumbo aligusia Ushauri aliotoa Mbunge Lugangira wa
kuandaa Kanuni za #FoodLabelling na kuahidi kuliangalia na kuondoa
mapungufu yaliyopo.