Mbunge neema lugangira aiuma sikio serikali suala la lishe shuleni

 

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania
Bara (NGOs) Neema Lugangira akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya
elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja
na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania
Bara (NGOs) Neema Lugangira akizungumza leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya
elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja
na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni 

 

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania
Bara (NGOs) Neema Lugangira amesema pamoja na serikali kuja na sera ya
elimu bure kwa kuweka uwekezaji mkubwa kwenye miuondombinu lakini iwapo
hawatatilia mkazo suala la lishe shuleni jitihada zote hizo zitakuwa
hatarini.

Aliyasema hayo
leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika Bajeti ya Wizara ya
elimu ,Sayansi na Teknologia huku akisisitiza umuhimu wa Serikali kuja
na mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe shuleni
kwa sababu kati ya watoto 45 kati yao 15 hawafundishiki kutokana na
tatizo la lishe duni.

Alisema
kwa sababu watoto wanapokuwa darasani lazima aweze kufikiri,kuchakata
,kuelewa ,kukariri anachofundishwa na mwalimu lakini kama ubongo wake
haufanyi kazi vizuri na hautajapata virutubisho sahihi mtoto huyo hawezi
kujifunza ipasavyo na hivyo ni sawa na kutegemea gari ambalo halina
mafuta liweze kutembea.

“Mh
Spika wanafunzi wengi wanatoka nyumbani alfajiri wanakuwa hawajala
wanakwenda shule wanashinda njaa akiwa darasani tumbo linanguruma kwa
sababu linakosa kitu cha kusaga na kupeleka kwenye ubongo kwa hiyo
mwanafunzi anakosa umakini kiasi kwamba mwalimu anatoka kufundisha
ukimwambie mwalimu kasema nini akasema sijui mtoto unaangaika kumpiga
kwa kusema ni mtoto mtukutu hana adabu hasikilizi darasani lakini ubongo
wake umesizi kufanya kazi kwa sababu ya njaa”Alisema Mbunge  Neema
Lugangira

“Lakini Mh
Spika ningependa kuikumbusha serikali kwamba  pia hali udumavu nchini
inachangia kwa kiasi kikubwa kwa watoto kutokuweza kufaulu na
kutokufundishika shuleni…wenzetu wataalumu wa lishe Tamisemi wanasema
kwamba  kila darasa la watoto 45 kati yao 15 hawafundishiki inaamaana
pamoja na jitihada zote hizo tunaendelea kufifisha jitihada kutokana na
uelewa ndio maana ufaulu unakuwa chini.”Alisisitiza Mbunge Neema
Lugangira

Mbunge Neema
Lugangira alisema kutokana na hali hiyo aliiomba serikali iweke mikakati
madhubuti kuhakikisha ya kila shule hususani za kutwa wanazalisha mazao
ya lishe ili kuhakikisha watoto hawashindi shuleni wakiwa na njaa.

 “Pia
niseme kwamba pamoja na jitihada zote za elimu bure,miuondinu bora
ikiwa bado tutaliweka pembeni suala la lishe shuleni jitihaza zote
zitafifisha malengo ya serikali ya kuhakikisha elimu yetu inanufaisha
watoto wa kitanzania kwa hiyo naiomba wizara ya elimu sayansi na
tenkologia ije na mkakati madhubuti tunakwenda kufanya nini kuhakikisha
watoto wanapata lishe shuleni”Alisema

Akizungumzia
suala la Hedhi Salama  Mhe Neema Lugangira alianza kwa kuipongeza
Serikali kwa mikakati waliyoweka kuhakikisha mtoto wa kike analindwa ili
apate elimu lakini mtoto huyo huyo kila mwezi anapofika wakati wa hedhi
anakosa siku tano mpaka saba.

Alisema
kutokana na  hali hiyo  anaiomba serikali itilie mkazo nafahamu kuna
bajeti ndogo ya elimu bure kupata msaada wa taulo za kike kwa dharura
lakini serikali iweke wazi lakini waje na mikakati madhubuti kwenye
eneo  hili.

“Kwa mfano
kwenye shule za msingi kuna wanafunzi wa kike 5,481,982 na sekondari wa
kike 1,284,410 kati ya hao wote tukichukulia asilimia 20 wapo kwenye
umri wa kubalee inamaana tuna jumla ya watoto 2,380,806 ambao kila mwezi
wapo hatarini kukosa shule siku tano mpaka saba hilo ni jambo nzito
inabidi wizara ilichukulie kwa uzito wa kipekee kuona namna ya
kukabiliana nalo”Alisema

Hata
hivyo Mbunge Neema Lugangira alisema lakini kwa wale wanaoenda shule
wanatumia vitu ambavyo ni hatari kwa afya zao kwa hiyo anaiomba serikali
ione namna gani inaweza kusaidia mtoto wa kike kwa kuhakikisha akosi
shule kwa sababu ya kuwa kwenye hedhi .

“Lakini
kwa kumalizia naamini kwa sababu Waziri ni Mama yetu na hayo masuala
yote mawili yanamgusa kama mama naamini atakuja na mpango mazubuti wa
kuhakikisha watoto wanapata lishe shuleni pia mtoto wa kike hakosi shule
kwa sababu anakuwa kwenye hedhi”Alisema

Kufuatia
suala hilo Spika wa Bunge Job Ndugai ameweza kulizungumzia ambapo
alisema kwenye suala la lishe kwa mfano maeneo mengi ikiwemo Jijini
Dodoma na maeneo mengine shule zina eneo kubwa  la kulima ya ardhi
lakini unakuta haina magunia mawili ya mahindi au mtama  kwa sababu ya
sera ya sasa watoto wasichangamke na kidogo na vijembe.

Spika
Ndugai alisema lakini katika maeneo yao ya shule wangeweza kila shule
kujipanga na kulima kwa kupata wastani wa magunia 50 hadi 70 kwa kuanzia
kabla ya hata wazazi wao hawajachangia chakula shuleni.

“Lakini
mtoto umechukua na umempeleka shuleni na mzazi umempungiza nguvu kazi
ya kufanya kazi nayo nyumbani amehaingaika peke yake na kiangazi
kikifika unamwambie mzazi achukule chakula apelekea shuleni hivyo ni
vitu vya kutazama kwani baadhi ya vitu ni kujipanga tu kwa sababu ardhi
ipo”Alisema Spika Ndugai