Mbunge neema lugangira ateuliwa balozi wa covid19

 

MBUNGE
wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akiwa na bango la
kuhamasisha uvaaji wa barakoa na wananchi kuhakikisha wanachanja

 

MBUNGE
wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 wa kwanza kulia
akiwa kwenye picha na Waziri wa Afya Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto
MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akifuatiwa na
Msanii maarufu
nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele
‘Steve Nyerere’ na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini,
Joyce Kiria.

Mbunge Neema Lugangira  ameteuliwa kuwa Balozi wa
harakati za kupambana na Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona
(Balozi wa UVIKO19 – COVID19).
Mbunge
Neema Lugangira  ameteuliwa  Alhamisi ya Agosti 12 mwaka huu na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Dk. Dorothy Gwajima Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na Mbunge Neema Lugangirq, wengine walioteuliwa ni Msanii maarufu
nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele
‘Steve Nyerere’ na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini,
Joyce Kiria. 
Tangu janga
la UVIKO 19 (COVID19) liingie nchini kwenye Wimbi la Kwanza hadi sasa
Wimbi la Tatu, Mbunge Neema Lugangira ameonyesha kupambana na janga
hilo huku akielimisha na kuhamasisha Watanzania kujikinga na kuchoma
Chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari duniani wa COVID19.