Mbunge wa rombo, joseph selasini ajiuzulu nafasi ya mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni

Mbunge
wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini  amejiuzulu wadhifa wa Mnadhimu wa
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni  kutokana na kutotambulishwa rasmi kwa
uongozi wa Bunge tangu ateuliwa miaka miwili iliyopita.


Selasini aliteuliwa kukaimu wadhifa huo
miaka miwili iliyopita, kufuatia aliyekuwa akishikilia wadhifa huo,
Tundu Lissu kuwa katika matibabu nje ya nchi baada ya kushambuliwa kwa
risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 nyumbani kwake
Jijini Dodoma.