Mchungaji rwakatare ‘mama kisulisuli’ asema vijana hawataki kuoa kukwepa majukumu,wengi ni marioo

Mama wa upepo wa kisulisuli na Askofu wa Kanisa la Mlima wa Moto Dkt
Getrude Rwakatare, ameeleza sababu ya wanawake wengi kushindwa kuolewa
ni kutokana na vijana wengi kukwepa majukumu yao.
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital,Askofu Dkt Getrude Rwakatare,
amesema kila mtu lazima aolewe na kuoa sio vijana kukwepa majukumu na
kukimbilia kuwa Marioo.
“Tatizo la wanawake kukawia kuolewa ni tatizo la kidunia, ulimwenguni
kote kuna tatizo kama hilo kwa sababu Wanawake tupo wengi kuliko
wanaume, lakini tatizo hili limekuwa kubwa zaidi kwa sababu vijana
wanakwepa majukumu yao ndiyo maana inakuwa shida” amesema Mama
Rwakatare.
“Vijana wa sasa hivi wengi wanakwepa majukumu hawataki kujiingiza kwenye
shida wengi wao ni “Marioo” wanataka kuolewa na majimama hii mbaya sana
na ndoa ni mipango ya Mungu” ameongeza.
Aidha Mama Rwakatare, amesema ndoa hazidumu kwa kuwa watu wanakaa mwaka
mmoja, mitatu au wengine ni miezi sita kisha zinakufa kwa sababu
maadili hakuna na sasa hivi watu wanaoana kwa ‘fashion’.

 Chanzo – EATV

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *