Mchunguzi mkuu takukuru amwandikia barua dpp kukiri makosa yake

Mchunguzi
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas
Batanyika (44) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo
kushawishi rushwa ya zaidi ya Sh. milioni 300, kupokea na kutakatisha
Dola za Marekani 20,000 amedai mahakamani amemwandikia barua Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) ya kukiri makosa yake.


Batanyika
alitoa madai hayo jana kesi yake ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa mbele
ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevini Mhina, katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, mshtakiwa alidai kuwa amemwandikia barua DPP na kwenye makubaliano anasubiri majibu ndugu zake wanafuatilia.

Hakimu Mhina alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 15, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *