Meya mhe. masumbuko ahimiza wazazi na wadau kuwafundisha watoto kutoa taarifa za ukatili manispaa ya shinyanga.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan
Masumbuko amewasihi wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuwafundisha watoto
kutoa taarifa za viashiria vya ukatili na uharifu ambao wanakutana nao.

Ameyasema hayo kwenye mafunzo yaliyoratibiwa na Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na shirika la Investing in Children and
Societies (ICS) ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo walimu walezi pamoja na
wanafunzi wajumbe wa baraza la watoto Wilaya ya Shinyanga ili kupunguza au kumaliza
vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mstahiki meya pamoja na mambo mengine amewakumbusha wawezeshaji
katika mafunzo hayo kuona namna bora ya kutoa elimu kwenye familia ili kutambua
umuhimu katika malezi ya watoto ili kuepukana na vitendo vya ukatili unaoendelea
kufanyika.

Mhe. Masumbuka amesisitiza wazazi, walezi pamoja na wadau
mbalimbali ambao wanatetea haki za watoto kuendelea kutoa elimu kwa
kuwafundisha watoto kutoa taarifa za viashiria vya ukatili na ukatili
wanaofanyiwa ili kutokomeza vitendo hivyo.

Amesema ni muhimu kuwafundisha watoto madhara yanayotokana  na vitendo vya ukatili ili kukua katika
mazingira salama ya kuishi huku akiwaomba wananchi kuhudhuria kwenye nyumba za
ibada ili kujengewa ufahamu zaidi katika kuepuka uovu.

“Kama
unaona kuna tukio siyo la kawaida popote pale toa taarifa wafundisheni watoto
kutoa taarifa, ukatili na uhalifu utaisha tukitoa taarifa toa taarifa badala ya
kunyamaza na kusema hayakuhusu nanyi walezi myaishi hayo mnayoyafundisha”
ameongeza
Mhe. Masumbuko.

“Siku
hizi tumekuwa na watoto wasio na adabu, vijana wasio na adabu lakini pia wazee
wasio na adabu kutokana na mambo kadhaa ukiwemo utandawazi unakuta wazazi
hawaelewani, wanagombana mbele ya watoto, hali hii inasababisha watoto wetu
waige tabia za ajabu , wasiwe salama nidhamu ya watoto inatakiwa ianzie ndani
ya familia ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama muda wote”,
ameeleza
Mh. Masumbuko.

“Tuwe
wabunifu ili watoto wetu wawe salama, tuwe wawazi tuwaeleze watoto ukweli
kuhusu madhara ya matendo ya hovyo tuhakikishe tunasimamia mafundisho sahihi na
maadili mema ili watoto wetu wawe salama na jamii iepukane na vitendo vya
ukatili wa kijinsia na maovu kama vile ushoga na usagaji”,
amesema
Mhe. Masumbuko.

Kwa upande wake, Afisa Elimu ya
Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Divisheni ya Sekondari Manispaa ya
Shinyanga, Beatrice Mbonea ameelezea mafunzo hayo huku akisema matarajio baada
ya walimu hao na wanafunzi kupata elimu juu ya ukatili.

Amesema maratajio baada ya
mafunzo hayo ni walimu kwenda kufanya mabadiliko chanya kwa kubaini wote
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ama watoto ambao wapo kwenye mazingira
hatarishi.

Aidha amewaomba wazazi na
walezi kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao ili kubaini changamoto
zinazowakabili hasa wawapo shuleni.

“Watoto
wengi wanakuwa katika mazingira hatarishi kutokana na wazazi kuwa na shughuli
nyingi ‘Busy’, kutojali na kutotenga muda wa kuongea na watoto walimu ni
wachache wameachiwa mzigo wa kulea wanafunzi wengi, wanaelemewa hivyo wazazi
wanatakiwa kushirikiana na walimu na majirani kulea watoto lakini ni lazima
wazazi wajitahidi kuwajua marafiki wa watoto wao”
,amesema Mbonea.

“Tuendelee
pia kuhamasishana kuhusu kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa shule za
sekondari ili kuepusha na vishawishi wanavyokutana navyo watoto wawapo njiani
kwenda au kutoka shuleni”,
 amesema.

Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Investing in Children and Societies
(ICS) wameendesha mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya
shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto
Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo yameanza  Jumanne Mei 16,2023  na yamehitimishwa leo Mei 17,2023 katika
ukumbi wa Mama wa Mama Samia uliopo shule ya Msingi Buhangija mjini
  Shinyanga.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan
Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto
ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan
Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto
ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan
Masumbuko akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto
ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga

Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya
shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga yakiendelea katika ukumbi
wa Mama Samia uliopo shule ya Buhangija mjini Shinyanga.