Mgeja amfyatua benard membe kauli zake tata…adai hazilingani naye afuate nyayo za lowassa

Khamis Mgeja

Na Paul Kayanda-Kahama


MWENYEKITI wa taasisi yaTanzania Mzalendo Foundation Khamis Mgeja
amemshauri aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa
Kimataifa katika serikali ya awamu ya nne Benard Membe afuate nyayo za
Waziri mkuu mstaafu Mhe. Eduard Ngoyai Lowassa kuiga mfano wake wa kuwa
na ustaarabu na uungwana wa kisiasa na akubali yaishe.Mwenyekiti huyo wa taasisi hiyo inayoshughulika na masuala ya haki,
Demokrasia na Utawala Bora, Mgeja amesema Membe amekuwa akitoa matamko
mbalimbali yaliyojaa ukakasi, maudhi, dharau, kiburi, kejeli, vijembe
pamoja na kujiamini kulikopitiliza na kuongeza kuwa amekuwa akimfuatilia
mara kwa mara kauli zake anazozitoa kupitia vyombo vya Habari pamoja
na mitandao ya kijamii Twitter. Mgeja aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari
kijijini kwake Nyanhembe Kata ya Kilago Halmashauri ya mji wa Kahama
mkoani Shinyanga ambapo alizungumzia kauli tata za mara kwa mara za
mwanachama wa CCM Benard Membe alizozitoa hivi karibuni na kudai kuwa
kauli hizo zimekosa uadilifu ndani ya chama na serikali pamoja na utu na
heshima kwa mtu aliyejaa imani za dini.Pia mwenyekiti huyo wa taasisi ya Mzalendo Foundation , Mgeja alitolea
mfano wa kauli tata zilizojaa ukakasi alizotoa hivi karibuni Waziri
huyo wa zamani katika serikali ya awamu ya nne Membe kuwa “BORA UFE
UMESIMAMA KULIKO KUISHI UMEPIGA MAGOTI HAYUKO TAYARI KUOMBA RADHI”.Mgeja alisema kuwa Membe amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na kupata hadhi ya kuwa mwanadiplomasia lakini kauli
anazozitoa hazilingani na hadhi yake kama mwanadiplomasia wala mtu
aliyeishi na imani ya dini utu na uungwana.“Mfano wanadiplomasia kama Membe wote Duniani hupenda kufanya kazi za
kupigania maridhiano na mapatanisho na pale wanapokoseana huwahi
kuombana radhi inasikitisha kuona matendo na kauli anazoto marakwa mara
Membe inawezekana kabisa hakuiva vizuri katika masuala ya Diplomasia,”
alisema mwenyekiti wa Mzalendo Foundation Khamis Mgeja huku alitolea
mfano.Mgeja alisema kauli nyingine tata ya Membe kama mwanachama wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kupitia mtandao wake Twitter amediriki kusema kuwa CCM
imekatika vipande na kama kanga haiwezi tena kushoneka.Aidha Mgeja alisema, Membe kama mwanachama hai wa CCM hakustahili kabisa
kutoa maneno hayo labda awe rangi mbili aliyejificha kwa kimvuli cha
CCM na kauli hizo zinamvunjia heshima na uadilifu mbele ya chama chake
na kumuondolea hadhi na heshima ya mwanadiplomasia na kugeuka hivi sasa
kuwa mwanaharakati.“Nimkumbushe Membe kuwa CCM hivi sasa inavyoonekana ni kwa vitendo iko
imara sana kama ilivyokuwa siku za nyuma enzi za baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere wote tumeona mageuzi makubwa CCM iliyoyafanya
ndani ya chama chini ya mwenyekiti wa Taifa Dk. John Pombe Magufuli na
sekretelieti nzima ikiongozwa na katibu mkuu Dk. Bashiru Ali ndiyo maana
mimi Mgeja na Mheshimiwa Lowassa na wengine tuliamua kurudi CCM ili
kuja kushirikiana kwa pamoja tukiwa ndani ya CCM kujenga nchi yetu kwa
maendeleo ya Taifa, na tulikubali yaishe,”alisema Mgeja.Mgeja alimfahamisha Membe kuwa uimara wa chama ni kuona serikali yake ya
awamu ya tano inavyotekeleza ilani kwa weredi na kwa kiwango cha hali
ya juu sana katika miradi mikubwa inayotekelezwa hivi sasa hasa katika
upande wa sekta mbalimbali za miundo mbinu, Reli, Ndege, barabara,
usafiri majini uboreshwaji wa huduma za jamii kama afya elimu, umeme
maji kilimo, uvuvi, ufugaji, sekta ya mali asili na utalii, sekta ya
Madini, viwanda pamoja na kupiga vita ubadhilifu wa mali za umma.Pamoja na mambo mengine Mgeja alisema kuwa kwa uzoefu wake katika
masuala ya kisiasa anavyomuona Membe njia anayoenda nayo na kupitia
katika harakati zake za kisiasa zilizojificha haziwezi kumfikisha popote
pale kwa kujitafutia umaarufu wa siasa nyepesi ni vyema asome alama za
nyakati na atambue kila zama na kitabu chake, watanzania wa leo
hawadanganyiki na kwamba anampa ushauri wa bure akatafute kazi nyingine
ya kufanya hata kilimo kitamsaidia.Mgeja alisisisitiza katika ushauri wa bure kwa Membe anawajibu kama
mwana CCM na wenzake waliojificha nyuma yake ni vyema na busara wakubali
yaishe tu na wapate muda mrefu wa kuzungumzia kwa wananchi mafanikio
yote mazuri yanayofanywa na serikali ya CCM ya awamu ya tano.Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *