Mh. luhaga mpina aibua sakata la tembo kuvamia wananchi, ataka wafugaji walioshinda kesi mahakamani kutendewa haki

 

MBUNGE
wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema Jimbo la Kisesa linachangamoto nyingi
sana ikiwemo uvamizi wa tembo ambao wamekuwa wa muda mrefu bila kupata
suluhisho kutoka serikalini.

Amesema
wananchi wanavamiwa na tembo mazao yao yanaliwa yakiwa shambani na hata
yakiwa nyumbani chakula kinaliwa mashamba yote yanakanyagwa watu
wamepoteza maisha wengine wamepata ukilema wa kudumu.
Mhe.
Spika tumelalamika sana na tumeomba sana serikalini kulitatua hili
tatizo lakini leo miaka mitatu sasa wananchi hao bado wanaendelea kwenye
dhiki kubwa sana ya uvamizi wa tembo lakini uvamizi huu uko kwenye
maeneo mengine pia
Mhe.
Waziri Mkuu kwa sababu ni muda mrefu sana na tumekuwa tukipeleka
malalamiko haya serikalini na hayajatatuliwa mpaka sasa hivi ambapo
imepeleka umasikini mkubwa kwa wananchi tunaomba tatizo hili lifike
mwisho.
Mhe.
Spika tunajua Serikali hii tuliyonayo ya awamu ya tano na hii ya sita
imetatua mambo mengi yaliyokuwa yameshindikana lakini imeweza kuyatatua
mambo makubwa imeweza kuyatatua haiwezi kushindwa kuwazuia tembo.

Mhe.
Spika tumeweza kumaliza mambo ya rushwa na ufisadi, tumeweza kumaliza
madawa ya kulevya tumeweza kumaliza ujambazi na ujangili, tumeweza
kumaliza uvuvi haramu tuje tushindwe na tembo”?
Mhe.
Spika hapa kuna mtu mmoja hajawajibika sawasawa tunataka safari hii
wananchi waishi kwa amani katika maeneo yao na tatizo hili la Tembo Mhe.
Waziri Mkuu agiza likomeshwe mara moja.
Mhe.
Spika tunalo tatizo pia kubwa sana la wafugaji ambao walikuwa wanafuga
wakakamatwa na wahifadhi kwamba wanachungia ndani ya hifadhi na baada ya
hapo wakaenda kushinda kesi mahakamani wakakatiwa rufaa wakaenda
kushinda kesi mahakamani zaidi ya wafugaji 30 wenye ng’ombe wasiopungua
5,000 ng’ombe wao mpaka sasa hivi wanashikiliwa na Serikali licha ya
kushinda kesi mahakamani.
Na
wamefuatilia serikalini kurudishiwa mifugo yao kwa sababu wameshapewa
haki hiyo na Mahakama warudishiwe mifugo yao lakini mpaka sasa hivi
tunavyozungumza Mhe Spika ng’ombe hao hawajarudishwa na sababu za
kutorudishwa hazijulikani mtu ameshinda kesi mahakamani kwanini uendelee
kuzuia mifugo yake?.
Mhe.
Spika kwa Jimbo la Kisesa peke yake ni zaidi ya ng’ombe 1,000
wanashikiliwa licha ya wananchi hao kushinda kesi mahakamani wananchi
akina Malimi Sendama na wenzake, Ndaturu Malolo, Kwandu Malaba, Masunga
Mhamali, Subi Maduhu na wengine Mhe. Waziri Mkuu tunataka kuambiwa huko
Serikalini aliyekataa ng’ombe hizi zisitolewe ni nani kama mahakama
imesha grant haki hao wafugaji aliyekataa huko serikalini ni nani?.
Mhe.
Spika namuomba sana Mh. Waziri Mkuu aliingilie kati hili suala
tukatende haki kwa hao wananchi wanyonge ambao mifugo yao imeshikiliwa
na Serikali licha ya wao kushinda kesi mahakamani na tukitoka kwenye
hili bunge niende na hizo ngombe za wananchi hawa