Miaka minne ya rais magufuli madarakani | tunaendelea kujimwambafai na mafanikio makubwa ya serikali yake

Makala Imeandaliwa na; Robert PJN Kaseko
Leo
ni Kumbukumbu Muhimu sana  Kwetu Watanzania tokea Kipenzi Chetu Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt J.P. Magufuli na Makamu wake
Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan waingie Madarakani Mnamo tarehe 05
Novemba, 2019. Na leo Wametimiza Miaka Minne (4) ya Utumishi wao.


Kama
Taifa, tunajivunia Utumishi wao Uliotukuka na Kwa Muda Mchache Tumepata
Mafanikio Makubwa sana Katika Kuitekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Rais
Magufuli na Serikali yake wamefanya Kazi Kubwa sana ya Kufanya
Mapinduzi Makubwa Katika Sekta zote na Kuleta Maendeleo zaidi ya
Matarajio ya wengi ( Beyond Expectations ). 

Baada
ya Rais Magufuli Kuingia Madarakani pamoja na Serikali yake wengi
walibeza na kusema tulishazoea na  hawana jipya, wapiga madili, Mfumo wa
CCM na Serikali utambana hata kama alikuwa Mtendaji Mzuri Katika Nafasi
ya Uwaziri, akiwa Rais hawezi kufanya lolote eti ni sawa na Mtu
yuleyule

 

Mzee
Mwenye slogan yake ya Hapa Kazi alipoanza Kupindua Meza na Kuchomoa
betri ameushangaza Ulimwengu. Walisema nguvu ya soda lakini mpaka leo
anatembea Katika Kasi ileile, Hadi leo Kazi Kubwa imefanyika Katika
Taifa letu, Miradi Mikubwa imeendelea Kutekelezwa Nchini.

Naomba nikutajie sehemu ya Utekelezaji huo;
Ujenzi
wa Mradi Mkubwa wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere ( Megawati 2115 )
Stiggler’s Gorge –  Mto Rufiji ( Utagharimu zaidi ya Trilioni 6.5 hadi
kukamilika kwake Ikiwa ni Kodi za Watanzania ),  Serikali imefanya kazi
kubwa ya Kulihuisha na Kuliimarisha Shirika la Usafiri wa Anga ( ATCL )
Ikiwa ni Moja ya  Mikakati Muhimu wa Kuimarisha Uchumi Kupitia Sekta za
Usafiri wa Anga na Utalii. 

Jumla
ya Ndege Saba Mpya zimenunuliwa Kwa Mabilioni ya Pesa yatokanayo na
Kodi za Watanzania; Bombardier 3, Airbus 2 na Dreamliners 2 ) 💪🏼 Ndege
zote zimekodishwa Kwa Shirika letu la ATCL na Biashara inaendelea
vizuri sana.


Tunajivunia
Mapinduzi Makubwa yaliyofanywa na Rais Magufuli na Serikali yake Katika
Sekta ya Afya ambapo Ule Mpango wa Kujenga Vituo Vya Afya Kila Kata
Nchini, Hospitali za Wilaya/Halmashauri  na Rufaa Kwa maeneo yasiyo na
Huduma hizo unaendelea Kutekelezwa kisawasawa. Zaidi ya Vituo Vya Afya 
300  Vimejengwa na Baadhi kukarabatiwa/ Kuboreshwa. 

Hospitali
za Halmashauri/ Wilaya 67 Zimejengwa nk. Mradi wa Ujenzi wa Mradi wa
Barabara za Juu/ Daraja la Juu Ubungo ( Ubungo Interchange ) Mradi
utakao gharimu zaidi ya Bilioni 200 Pesa za Kitanzania na Maendeleo ya
Mradi ni zaidi ya 50% – Mbioni Kukamilika, Mradi wa Ujenzi wa Daraja
Ziwa Afrika Mashariki ( Ziwa Victoria ) litakalo unganisha Mikoa ya
Geita na Mwanza ( Busisi – Busisi ) Kilomita 3.2, Mradi huu umepangwa
kugharimu Bilioni 699.9 Pesa za Kitanzania hadi Kukamilika kwake, Juzi
nimepita Pale Mto wami Kazi ya Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Mto Wami
Inaendelea. 

Jumla
ya Bilioni 71.4 Pesa za Kitanzania zitatumika Kukamilisha Mradi huu
ambapo pia Barabara yenye urefu wa Kilomita 4.3 ya Lami itajengwa kila
upande wa Daraja hili la Mto Wami kutokea hapo.( Ni kazi tuu hakuna
kulemba 💪🏼).


 Tusisahau
Miradi Mikubwa ya Kuimarisha Miundo mbinu wezeshi  ya Uchumi
inayoendelea kutekelezwa na Serikali hii ya Awamu ya Tanu Chini ya Dkt.
John Magufuli. 

Mfano
Serikali kupitia TARURA na TANROADS imeendelea Kujenga Barabara za Lami
zenye Ubora wa Hali ya Juu Kama ule Mradi wa Upanuzi Barabara ya Kumara
– Kibaha kwa Njia Sita  ( 19.2 Kilomita ) Mradi utakaogharimu zaidi
ya   Bilioni 140.44 Pesa za Kitanzania, Zile Barabara za Arusha za
Mchepuo ( Arusha By-Pass 42.2 Kilomita ) na Ujenzi wa Barabara za Njia
Nne Kutokea Pale Ngaramtoni hadi USA River 14.1 Kilomita na   ambazo
zimekamilika na zinatoa Huduma bora kabisa haja Jijini Kwetu Arusha.
Zaidi ya Bilioni 85 zimetumika Kuboresha Maisha ya Wananchi wa Arusha.


 Ebwana
Tusisahau Miradi Mikubwa ya Maji inayotekelezwa na Serikali yetu tukufu
Nchini Kote, Mfano mmoja miongoni mwa mingi ni huu Mradi wetu Mkubwa wa
Maji  Unaotekelezwa hapa Arusha utakaogharimu Bilioni 520 Pesa za
Kitanzania. 

Nimalizie
kwa kutaja iliyofanyika Katika Kufanya Mapinduzi Makubwa Katika Sekta
ya Nishati na Madini. Mabadiriko Makubwa ya Sharia ya Madini yamefanywa
na Bunge letu Tukufu ili kuhakikisha Madini yetu yanatunufaisha
Watanzania na niseme tu site tulishuhudia Sakata la Makinikia ambapo
hadi mwisho Wahusika tamka Kuilipa Serikali yetu Mabilioni ya Pesa kama
fidia dhidi ya Unyonyaji Mkubwa uliofanywa na Mabeberu.


Yapo mengi yaliyotekelezwa na Serikali ya Rais Magufuli toka Rais wetu ameingia Madarakani  Novemba 05, 2015. 

Kama Taifa Tumepiga hatua kubwa sana Kimaendeleo. Uchumi wetu umeendelea Kukua Kwa Kasi sana na Mambo yanaonekana Kwa Macho.


Watanzania
tusidanganywe na Upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya watu. Hawana
lolote zaidi ya Kutuvuruga na Ukweli ni Kwamba Watanzania tulikuwa na
Kiu kubwa ya Kuona siasa zetu zinabadirika na Kuwa siasa zinazojikita
katika Kuleta Maendeleo kwa Watanzania na Kutatua Changamoto na Kero
mbali mbali zinazo wakabili Watanzania, na Mungu ametujalia Kumpata Rais
ambaye akiahidi anatekeleza Kwa Vitendo, anachapa Kazi tu. 

Anasimamia
Vizuri sana Ukusanyaji wa Mapato na Matumizi ya Serikali. Anasimamia
VIZURI sana na kwa Uaminifu Mkubwa Raslimali za Taifa letu na
Kuhakikisha Zinawanufaisha Watanzania wa Sasa na Vizazi Vijavyo.


Rai
yangu kwa Watanzania wenzangu; Tumshukuru Mungu kwa Kutupatia Kiongozi
Mzalendo, Mchapa Kazi, Msikivu katika Kusikiliza na Kutatua Kero na
Changamoto za Wananchi wake, asiyetishika wala Kuyumbishwa, Jasiri na
Mwenye hofu ya Mungu. Tuendelee Kumuombea Rais wetu Afya njema, Maisha
Marefu na nguvu kubwa zaidi ya Kufanya Makubwa zaidi ya Haya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS MAGUFULI NA WASAIDI WAKE WOTE, AMEN.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
Novemba 05, 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *