Miili 16 ya waumini waliofariki wakikanyaga mafuta ya upako yatambuliwa…kuagwa kesho uwanja wa majengo

Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amesema miili ya watu 20
waliofariki kwenye kongamano la Mtume na Nabii Mwamposa, itaagwa kesho
Februari 3, 2020, kwenye viwanja vya Majengo mjini Moshi.  Amesema hadi
sasa tayari miili 16 imeshatambuliwa.


Kwa
upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro amewataka
Watanzania kuwa  makini kwani kinyume na hapo itakuwa shida sana na
kuongeza iko haja kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa kuanza
kuyafuatilia makanisa yote nchini na hasa makanisa madogo madogo ambayo
sasa yamekuwepo kila mahali.


“Sio
kila padri, mchungaji basi anataka kuwachunga kondoo wake waende kuuona
ufalme wa Mungu, wengine wanahangaika na utafutaji tu wa maisha.Sio
kwamba nahukumu lakini kuna mambo ya kujifunza,”amesema

Kuhusu Polisi iwapo walikuwepo kwenye kongamano hilo la Mwamposa, IGP
Sirro amesema ameshatoa maagizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimajaro
kufuatilia na iwapo walikuwepo polisi lazima waulizwe imekuaje hadi
watu wakapoteza maisha na wao wakiwepo, kwani sheria lazima ichukue
mkondo wake.