Mikoa ya kanda ya ziwa yang’ara matokeo ya darasa la saba 2019


Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania
(NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
ambako mikoa ya kanda ya ziwa imeonekana kuongoza.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo
Jumanne Oktoba 15, 2019 nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika orodha ya
shule 10 bora kitaifa zimeshikwa na wanafunzi kutoka katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa ikiwemo mikoa ya  Mara,Shinyanga,Kagera,Mwanza.

Kwa upande wa Watahiniwa bora kitaifa
nafasi ya Kwanza imechukuliwa na mtahiniwa kutoka mkoa wa  Mara,nafasi
ya pili Geita, nafasi ya tatu mkoa wa Dar es salaam (siyo Kanda ya
Ziwa),nafasi ya nne,tano,sita ni Mara, saba Shinyanga, nane Mwanza,tisa
Shinyanga na kumi Mara
.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *