Milioni 600 kujenga upya kituo cha afya lukole kilichoachwa na wakimbizi mkoani kagera.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.

Zaidi 
ya  sh milioni 600 Za kitanzania  zimetengwa na Halmashauli  ya  wilaya
ya Ngara  ili kujenga upya kituo cha afya Lukole kilichokuwa kimejengwa
kwa tope na kilichokuwa  kikiwahudumia wakimbizi waliokuwa wakiishi
katika kambi hiyo.

 
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya  wakimbizi  kutoka nchi jirani za Burundi na
Rwanda  waliokuwa wakiishi  kambini hapo kuondoka na kituo cha afya 
kuendelea kuwahudumia wananchi wanaoishi jirani na kambi hiyo.

 
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauli ya Ngara  Aidan Bahama   amesema kwa bahati
mbaya kituo  hicho kilijengwa  kwa tope na kupelekea  baadhi ya majengo 
Kuwa na hali mbaya na kuwa katika  hatari ya kuanguka.
 
Kadhalika
Aidan ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo na amemshukuru  mh rais
John Pombe Magufuli kwa kutoa pesa ambapo baada ya ujenzi huo kituo
hicho kitakuwa ni moja ya vituo bora wilayani Ngara.
 
Nao
baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika kituo hicho cha Afya Ambao ni
Bw Joseph Hezzron,bw James Charles,Bi Noral Charles Mihayo  wameipongeza
hatua hiyo ya serikali nakusema kuwa nijitihada za kujali huduma za
wananchi.
 
Mkurugenzi
huyo amebainisha kuwa Jumla ya majengo sita yatajengwa katika kituo
hicho ikiwa ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje,jengo la
upasuaji,maabara,jengo la kuhifadia maiti na nyumba moja ya mtumishi.