Mjukuu wa hayati mwalimu julius nyerere aliyekuwa anaishi shinyanga kuzikwa kesho butiama mkoani mara

Mwenyekiti wa mtaa wa Mabambase Bwana Seif Nassor Hemed akizungumza.Na Mapuli Misalaba, ShinyangaMwili wa Edward Majige Nyerere ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere umesafirishwa leo kwenda Butiama Mkoani Mara kwa Mazishi.Marehemu Edward Nyerere mwenye umri wa Miaka 26, alifariki dunia juzi siku ya jumamosi Novemba 11,Mwaka huu 2023 kwa ajali ya pikipiki aliyokuwa akiendesha,iliyotokea majira ya saa 12.00 asubuhi katika Barabara ya Uhuru eneo la Bushushu.Edward Nyerere alikuwa mtumishi wa NIDA Mkoa wa Shinyanga ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga. Akizungumza  mwenyekiti wa mtaa wa Mabambase Bwana Seif Nassor Hemed ambaye ameelezea namna alivyopokea taarifa za tukiola kifo cha marehemu huyo.Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi wameomba watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabara ikiwa ni pamoja na kuepuka mwendo kasi.Mazishi ya Edward Nyerere yanatarajiwa kufanyika kesho Jumanne Novemba 14,2023 katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara,mahali alipozaliwa.