Mkoa wa shinyanga wapata hati safi miradi iliyotembelewa na mwenge wa uhuru, rc mndeme atoa ahadi

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
amesema kasi ya usimamizi wa miradi ya maendeleo katika Mkoa huo itaendelea ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 2,2023 wakati
akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, baada ya kukamilisha mbio
zake  katika Halmashauri zote sita za
Mkoa wa Shinyanga.

Rc Mndeme amesema miradi 41 yenye thamani shilingi
bilioni 14.27 imeonwa, kuwekewa mawe ya msingi, kufunguliwa na kuzinduliwa  katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Mwenge wa uhuru umekimbizwa umbali wa kilomita
571.5 huku akiahidi kufuatilia na kuisimamia vyema miradi hiyo ikiwemo miradi
ambayo imewekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mwaka huu ili
iweze kukamilika kwa wakati.

“Kwa
niamba na uongozi wa Mkoa na wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuahidi kuwa
miradi yote iliyowekewa mawe ya msingi wakati wa Mwenge wa uhuru itafanyiwa
ufuatiliaji na usimamizi wa kutosha ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora
huku ikisingatia thamani ya fedha”.

 “Kwa miradi iliyozinduliwa na kufunguliwa tutahakikisha
kuwa inaendelea kutunzwa vizuri na kutumika kuleta tija na malengo
yaliyokusudiwa  kwa maendeleo ya umma kwa
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga aidha kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru
nakuhakikishia kuwa maelekezo yote uliyoyatoa kwenye miradi nitayasimamia
kikamilifu ili kuona utekelezaji wake unakuwa wa tija kwani katika Mkoa wa
Shinyanga chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hakuna kilichosimama”.
amesema
RC Mndeme

RC Mndeme amesema miradi
11 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 imewekewa mawe ya msingi, miradi 14
yenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 imezinduliwa, miradi 4 yenye thamani ya
shilingi bilioni 1.3 imefunguliwa huku miradi 12 yenye thamani ya shilingi
bilioni bilioni 1.5 imeonwa na Mwenge wa uhuru 2023.

Ameongeza kuwa jumla ya miti
450000 imepandwa katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na kufanyika
kwa  huduma ya upimaji wa VVU, Ukimwi,
Malaria, uchangiaji wa Damu salama pamoja na elimu kuhusu athari za madawa ya
kulevya.

Akizungumza kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Taifa
Bwana Abdalla Shaim Kaim amesema kuwa ameridhishwa na hatua za miradi mbalimbali
ya maendeleo katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwapongeza viongozi kwa usimamizi
mzuri wa miradi hiyo.

Mwenge wa uhuru ulipokelewa Mkoani Shinyanga Julai
27,2023 katika Wilaya ya Kishapu na kisha kukimbizwa katika Halmashauri zote
sita za Mkoa wa huo ambapo baada ya kukamilika kwa  mbio hizo Mkoa wa Shinyanga umepata hati safi
(Clean Sheet).

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela
amesema  katika Halmashauri sita za Mkoa
huo, Mwenge wa uhuru utakibizwa ubali wa kilomita 755.54 na kupita kwenye jumla
ya miradi 59 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 29.

Mwenge wa uhuru kwa Mwaka
2023 unaendelea kukimbizwa katika mikoa mbalimbali Nchini ukiongozwa na Bwana
Abdalla Shaim Kaim pamoja na kaulimbiu inayosema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na
uchumi wa Taifa.

Mwenge wa uhuru kitaifa
ulizinduliwa April mosi 2023 na kwamba mpaka sasa umekimbizwa katika mikoa 20 ambapo
Mkoa wa Geita ni Mkoa wa 21.

Mwenge wa uhuru ukikimbizwa baada ya  kuwasili Mkoani Geita kwa ajili ya makabidhiano leo Jumatano Agosti 2,2023.

Viongozi mbalimbali kutoka  Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Nyang’holongo wilaya ya Nyang’hwale mpakani mwa Shinyanga kwa ajili ya kukabidhi Mwenge wa uhuru Mkoani Geita leo Jumatano Agosti 2,2023.

Mkimbiza mwenge wa uhuru 2023 akiwa kwenye picha ya pamoja.

Burudani ikiendelea katika eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Nyang’holongo wilaya ya Nyang’hwale
mpakani mwa na  Geita.