Mkuchika asema wanaowahamisha watumishi vituo vya kazi kabla hawajathibitishwa atawashughulikia

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Kepteni George 
Mkuchika amesema atawashughulikia wale wote anaohamisha watumishi vituo
vya kazi kabla hawajathibitisha kwani ndio wanaochangia kuwepo kwa
changamoto ya baadhi ya Mikoa kuwa na upungufu wa watumishi.


Akizungumza
Jijini hapa jana wakati akizindua Baraza Kuu la nne la Wafanyakazi
katika Utumishi wa Umma Kepteni Mkuchika amewataka utumishi wa Umma
kutambua kuwa kila wakati wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi mahali
popote kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Amesema
katika ziara yake Mikoani amegundua Mikoa ya pembezoni ina uhaba mkubwa
wa watumishi, akitolea mfano Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ambayo ina
watumishi chini ya asilimia 50.

Kuhusu
suala la Rushwa, amesema taasisi zilizopo chini ya Ofisi Rais
zinatakiwa kuwa kioo katika kukema vitendo vya rushwa, kwani Ofisi hiyo
ndio inayoshughulikia wasiowaadilifu na si kujihusisha na vitendo hivyo.

Kwa
pande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Leah Ulaya amesema
watumishi wa Umma wanajua kazi kubwa inayofanywa na Rais katika kuleta
maendeleo kwa wananchi hivyo wataendelea kufanyakazi kwa weledi na
uadilifu ili kuunga mkoni juhudi za Seriali.

Kuhusu
malalamiko yaliyopo kwa watumishi wanaopandishwa madaraja lakini
kiwango cha mshahara hakibadiliki,Wizara hiyo amewahakikishia kuwa suala
hili litapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo, huku ikimesema kuondolewa
kwa watumishi 19,708 waliobainika kuwa na  vyeti vya kughushi kupitia
zoezi la uhakiki kumeifanya Serikali kuokoa kiasi cha Sh 19.838 bilioni.
Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *