Mkurugenzi wa bsl mr. black awajengea uwezo wanachuo wa shycom kuhusu nyanja na stadi za usahili.

Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkurugenzi
wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black ametoa
mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa chuo cha ualimu Shinyanga SHYCOM kuhusu
Nyanja na stadi za usahili.

Mafunzo
hayo yamefanyika katika ukumbi wa SHYCOM na kuhudhuriwa na wanachuo pamoja na
baadhi ya hamasa wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mr.
Black pamoja na mambo mengine amefundisha Nyanja na standi za usahili
(Interview Skills) jinsi ya kuomba ajira kwenye taasisi za serikali pamoja na
taasisi binafsi.

“Kabla
hujaanza kutafuta kazi kwanza lazima ujue umesemea nini ama unauwezo wa kitu
gani lakini pili jitahidi kufahamu je ulimwengu unahitaji nini kwa sasa lakini
pia tunaangalia sera ya Nchini imeelekeza nini lakini pia jiulize kabla ya
kwenda kutafuta ajira je unataka mkataba wa muda mrefu au muda mfupi unaweza
kupewa mkataba wa Miaka kumi kumbe lengo lako ni kupata mkataba wa Miaka mitano
tu”.
Amesema Mr. Black

“Tunapokwenda
kutafuta kazi tunakutana na kitu kinachoitwa usahili wa kazi babla ya kuingia
kwenye chumba cha Interview kuna hatua tatu lazime uzingatie kabla hujaingia
kwenye chumba cha usahili ufanye nini unapokuwa kwenye chumba cha usahili
ufanye nini na baada ya kutoka kwenye chumba cha usahili ufanye nini”

“Interview
ikitangazwa saa nne kamili hakikisha wewe unafika saa tatu kamili unapokuwa
umejiandaa kwenye interview usipendeze sana lakini pia usikele sana na
usiikamie sana jiamini jibu maswali yote unayoulizwa  taratibu na usipaniki maana kuna maswali
mengine ya mitego kutaka kujua wewe unauwezo wa kutunza siri za taasisi au
kampuni na ukiona swali hulifahamu siyo dhambi kukumbali kwamba sahamani swali
hili silifahamu ila mtakaponipa nafasi kwenye hii kazi litajitahidi nifahamu”
Amesema
Mr. Black

Aidha Mr. Black amefundisha jinsi ya
kujiajiri na uanzishaji miradi ya kielimu, utafutaji mtaji na hatua sahihi
katika utafutaji ajira kwa wanachuo hao wa chuo cha SHYCOM.

Baadhi ya wanachuo wa chuo cha ualimu
Shinyanga (SHYCOM) wamesema watafanyia kazi hayo yote waliyofundishwa huku
wakipongeza na kuishukuru taasisi ya The BSL kwa kutoa elimu hiyo.

Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company
Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black ametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo
vijana wa chuo cha SHYCOM na kwamba semina na mafunzo hayo ni endelevu katika
Mkoa wa Shinyanga

 

Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company
Limited na BSL Schools Tanzania Mr. Black akitoa mafunzo kwa baadhi ya
wanafunzi wa chuo cha ualimu SHYCOM Manispaa ya Shinyanga.

 

Semina ya  mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa chuo cha
ualimu Shinyanga SHYCOM kuhusu Nyanja na stadi za usahili ikiendelea kutolewa
na Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania
Mr. Black